Thursday, May 20

Karibu Jenipher

Mama na Mwana kwa niaba ya wadau wooote tunafuraha ya kumkaribisha mdau mpya aliyezaliwa tarehe 5, May mwaka huu, pale hospitali ya Bugando, Mwanza.

Wazazi wake wana .furaha kubwa kwa ingizo hili jipya la furaha kwenye maisha yao. Mdau amepewa jina la Jenipher. Picha hizo juu mbili ni muda mchache, kama dakika tano tu, baada ya kuzaliwa.

Mdau pia ana kaka anayeitwa John, kwa hiyo mama yao, Emmy siku hizi unaweza kumwita Mama J's. Naona baada ya kuulizia watoto no 2, napewa majibu ya vitendo, si maneno, kumbe wadau walikua njiani.
Hapa ni siku ya pili baada ya kuzaliwa...beautiful...Mungu amjaalie mdau na mama mtu afya njema na maisha yenye kheri na baraka tele.

No comments: