Tuesday, May 25

Tangazo la utoaji mimba kwenye Tv

Shirika la afya ya uzazi, ambalo pia lina clinic hata hapa nchini, Marie Stopes limetengeneza tangazo la televisheni kuhusu huduma za utoaji mimba.

Tangazo hilo litakalorushwa Uingereza (kasoro Ireland ambako kutoa mimba ni kosa) kuanzia wiki ijayo linauliza 'ARE YOU LATE ?' likimaanisha umechelewa siku zako?

Ingawa limeshaanza kuzua maswali mengi hasa kwa wanaharakati wa kupinga utoaji mimba, wenyewe Marie Stopes wanasema kuwa nia sio kuwaamasisha watu watoe mimba, bali kuwapa wanawake waliopata mimba bila kupanga ushauri usioegemea upande wowote na hivyo kumpa mwanamke huyo nafasi ya kuchagua kutoa au kubaki na hiyo mimba akiwa na taarifa sahihi.
2 comments:

Mgumba said...

Jamani hizo mimba wanazotoa ningeipata mimi hata moja tu..God only one kid...oh!! Mungu naomba uwanyime kizazi hao wanaotoa mimba zilete kwangu!!

Anonymous said...

SAsa marie stopes wamehalalisha kutoa mimba kisheria au maana navyojua mimi mimba TZ ni criminal au sheria zimebadilika jamani tuambiane maana isije ikawapotosha watu we need to know more about this program ya marie stopes nimeshitushwa sana.