Wednesday, June 16

Happy birthday Jerry

Leo mdau Jordan anatimiza miaka minne (4).
Mama na Mwana pamoja na wadau wooote tunamtakia Jordan maisha mema, marefu yenye kheri na fanaka tele, Mungu amjaalie sana.  
 
*****
 Hii ni message toka kwa ma'mtu:

Hi, Mama na mwana
Naitwa Tumaini, napenda kukutumia details za mwanangu Jina lake JORDAN (Jerry) watoto wenzie wanapenda kumuita hivyo sababu ya utundu wake. Kesho ni Birthday yake anatimaza miaka 4. namwambia nampenda sana japo niko mbali nae. Namuombea kwa mungu ampe uzima na furaha milele Natamani angekuwa pembeni yangu tukicheza asijali ni majukumu tu lakini avumilia siku moja nitakaa pembeni yake namuandalia maisha tu. Me niko Zanzibar yeye yuko Rukwa (Sumbawanga). Ampende bibi yake maana ndo mama yake tangu akiwa na miaka miwili mpaka sasa anatimiza miaka 4. kesho 16/06/2010. HAPPY BIRTHDAY. I LOVE HIM SO MUCH.  Aende shule hata akikorogewa uji wa sembe wa lishe atakunywa jioni kwa bibi yako.

No comments: