Friday, July 23

KWELI HII NI HAKI?

Habari za kazi? Pole na majukumu.naandika email hii nikiwa na machungu mengi sana na nahitaji msaada hata wa mawazo kupitia kwenye blog yako.

Mimi ni mjane,mume wangu alifariki miaka  kama mitatuiliyopita,niliachwa na mtoto ambaye sasa hivi ana miaka 8.Nashukuru mungu sikupata matatizo wala bugudha kutoka kwa wakwe zangu wala shemeji na mawifi usimamizi wa miradhi waliniachia mwenyewe.

Sasa basi hapa ndo tatizo linapoaanzia ndo maana naomba ushauri,kwanza kufungua miradhi kwenyewe pale mahakamani ilikua ni kero maana niliombwa rushwa vya kutosha maana nilikuwa muhitaji nikatoa ili nipate haki za mume wangu nikijua ni mwisho kumbe  bwana ndo ilikua mwanzo wa movie nzima,sasa basi kila kona ukiiingia unaombwa maji ya kunywa hadi napata cheque bado ikawa shida ilivyoenda Mahakama kuu ndo kabisa eti wanaomba laki 3.

Swali langu ni kwamba hivi hawa watu hawana huruma na mimi MJANE AMBAYE NIMEACHWA NA MTOTO ANAYENITEGEMEA??

Niliwaambia wanipe cheque zangu then nitawapa hela baadae,Ahsante Mungu nilipata haki yangu sasa bado
wale watu wananipigia simu kunisumbua vipi hela yetu kama vile wananidai.Hivi wanadhani mimi sina la maana cha kufanyia hiyo hela niliyoachiwa na marehemu mume wangu?

Jamnai naombeni mawazo yenu kweli hii ni haki? Binafsi naumia sana kila wakinipigia simu saa nyingine najisikia hata kuwajibu vibaya.

Naombeni maoni yenu jamani.
Ahsante ...

11 comments:

Lydia said...

Pole sana Aunt, sasa la kufanya ni kuwashtaki hao watu sehemu husika, kukupa wewe cheque ni kazi yao ambayo wanalipwa mshahara kwayo.

Mi naomba wasikusumbue kabisa wala kukunyima raha, na hao walokwisha kula pesa yako natamani nao wangechukuliwa hatua, wamezoea sana kula jasho si lao.

mungu akusimamie kwa kila jambo.

Anonymous said...

dada lakini si uliwaahidi mwenyeku kuwa utawapa? we wape tu yaishe.... Mungu atakulipia!

Anonymous said...

Bongo kila kitu rushwa!!!ndio maana hatuendelei!

Anonymous said...

pole dada, ila usiwape hata senti, kwani walikuwepo wakati unahangaika kutafuta na mumeo? afadhali hata uwape ndugu zenu kuliku hao wasiokuhusu!!!

Anonymous said...

Badili namba ya simu na achana nao na hao wafedhuli wanuka rushwa wasio na haya...

Anonymous said...

usibadili namba ya cm, bora uwa rekodi na kuwashtaki kwenye vyombo husika(ila nakutakia kila la kheri usijaukaenda kushtaki nao wakataka kitu kidogo!) na hao wanao kwambia uwape wanakupotosha dear! maana mhini na mhiniwa njia yao ni moja, ukitoa wewe rushwa is as bad as kupokea rushwa! saidia jamii name and shame watu hao... warekodi tu ili uwe na hard evidence...

Dawa ya hao watu ni kuwaripoti TAKUKURU(PCCB)katika ofisi yoyote iliyokaribu nawe(kila wilaya na mikoa nchi nzima) na kwa DSM kuna ofisi TEMEKE maeneo ya BORA kwenye kona ya kwenda uwanja wa Taifa,KINONDONI zipo magomeni mapipa ghorofa karibu na kituo ch daladala za kwenda ubungo, ILALA ofisi zipo mtaa wa shauri moyo kwenye jengo lenye ofisi za TRA na kuna ofisi kwenye kona ya mtaa wa Samora/Mkwepu,au nenda ofisi za Makao Makuu zilizopo UPANGA mtaa wa KALENGA,ni karibu na TAMBAZA SEKONDARI.Njia nyingine wapigie namba 113(simu ya bure)au 022 2150041/6.Hapo utasaidiwa mamie.

Anonymous said...

Hakuna neno ninalolichukia kama mtu kujita Mimi mjane!! Eti sina mume!I hate that word,simama kwa miguu yako.Nawashauri wanawake wote mjifunze kujitegemea tangu kabla hata hamjaolewa!! MJANE MJANE MJANE!!!

Anonymous said...

Bora wewe mjane umeachwa na fedha za kumtunza mwanao. Wengine tulikataliwa na mimba matumboni na watoto tunawalea wenyewe.