Monday, June 7

Wikend hii tulikua beach

Baada ya kujenga taifa kwa wiki nzima, Jumamosi tukawaita wanafamilia tu-refresh nao beach.
Hapa Khloe Mfumu akiwa na Anko Collins Mtita, baada tu ya kuingia na ma'mtu, Rosemary Mallya.

X kama kawaida yake, alivyoona maji tu, akayakimbilia huku anasema 'oga, oga'
...ilikua full kukimbizana, mi nikiwa ndio ukuta kati yake na maji mengi!

...mawimbi nayo hayakua na huruma...

...mi nilikua nikiona wimbi la kumfunika namdaka!!!

...mwisho akakubali kutoka baada ya kuona baridi inazidi...

...pua ziliishiwa break!

...hapa alikua anatetemeka kwa baridi, akawa mpoleee, kama sio yeye aliyekua anang'ang'ania kwenye maji!

...wakati X akihangaika na bahari, Khloe alikua nchi kavu anakura raha mchangani, hapa anahangaika na miwani mikononi, na mpira!

... hapa yuko na ba'mtu, Innocent.

...hapa katuliaaaa mikononi mwa Aunti Ikunda...uzuri hakatai mtu!

...X baada ya kuvaa, wala hakutulia, akaanza kucheza mpira na Anko Collins...

...kidogo anahangaika kwenye mabembea...

...kwa ufupi watoto na wakubwa wote tuli-enjoy sana, yani tulimkosa baba tu, maana kasafiri, hadi bibi alikuwepo.
Hivi ndivyo nnavyopenda wikend yangu iwe, nicheze na X wangu hadi tuwe hoi, malaika wangu afurahiiii, ndio na mimi nnakua na furaha!

3 comments:

Grace said...

safi sana Jiang

Anonymous said...

Haa Ikunda, huyo mtoto amekupendezea sana kama wakwako vile...ha ha haaaa!

Anonymous said...

una akili sana wee dada,maana raha na family yako unazijua tena wala si za makuu...ubarikiwe bi dada

tunajifunza mengi humu