Wednesday, July 21

Baba na mama weusi...mtoto mzungu!!!

 (Familia nzima ikiwa na mtoto mpya aliyeshangaza kila mtu)
Maajabu ya ulimwengu. Wazazi wa ki-Nigeria, wanaoishi nchini Uingereza wamezaa mtoto mzungu, sio albino jamani, ni mzungu!

(Huyu ndiye Nmachi)
Mtoto huyo aliyepewa jina la Nmachi, lenye maana ya 'Uzuri wa Mungu' ameshangaza wengi, sio wazazi wake, mimi na wewe tu, bali hadi madaktari bingwa wa genetics (ndio vinasaba eehe?) kwa sababu wazazi wake, Ben na Angela, hawana chembe ya uzungu wala ndugu  wa kuvuta na kamba mzungu.

Mume mtu, Ben anasisitiza kwamba, anamwamini mkewe kwa asilimia 100, na anaseme, "Hata kama mke wangu angekua si mwaminifu, mtoto asingetokea hivi,"

Kuzaliwa kwa mtoto huyo kuliwaacha wazazi midomo wazi, wakibaki wanamwangalia mtoto kwa masaa kadhaa bila kusema kitu---pata picha ingetokea kwako ingekuaje???

Professor Bryan Sykes, mkuu wa kitengo cha genetics Chuo cha Oxford na anayeaminika Uingereza nzima ameita uzazi huo kitu cha ajabu, maana walishapima na kuona mtoto ni wa wazazi hao wawili, na pia mtoto huyo sio albino.
"Hii ingewezekana angalau kama wazazi wote wawili wangekua ni mchanganyiko, lakini hawa sio mchanganyiko kabisaaa," alisema mtaalam huyo, huku akiongeza kwamba hata nywele za mtoto huyo, ambazo ni za rangi ya blonde haziko kama za watoto wazungu mara wanapozaliwa, kwani zake ni nyeupe sana.
Kaka wa mtoto huyo mpya, ambaye ana miaka minne, haelewi, maana ba'mtu anaeleza, "Mtoto wetu wa kiume anakuja kila saa kumwangalia mtoto halafu anakaachini anaonekana kama kuna kitu kinamchanganya.

Wazazi hao wana watoto wengine wawili, huyo wa kiume mwenye miaka minne na wa kike mwenye miala miwili, amabo wote wamezaliwa hukohuko UK na ni weusi kama wazazi.

3 comments:

Anonymous said...

Kwa kweli ukiangalia kwa makini huyu mdhungu mswahili anafeatures zote za kiswahili isipokuwa rangi. ona pua lake domo macho then mlinganishe na baba mtu na huyu kaka mtu. Yawezekana imetokea tu Genetic disorder kwenye black pigments za skin akatokea hivyo.

Anonymous said...

mmmh, hapa mswahili mwenzetu kaliwa...hana chake!

Anonymous said...

mmh baba kaibiwa hapo