Wednesday, July 28

Msaada wa lishe ya mdau!

Hii nimetumiwa na mdau, najua hili suala linasumbua watoto wengi, maana ni wabishi kula, wachache sana wanapenda kula: 

Mimi shda yangu ni ndogo/kubwa mwanangu anaenda miezi tisa ila utata sana hapendi kula!sasa sijui ntatumia format gani ili awe mlaji!naomba mwngozo!

Wale wa wanaopenda kula tusaidieni hapa.

3 comments:

emu-three said...

Miezi tisa tu, wangu sasa ana miaka saba, lakini kula mpaka mshike fimbo, nafikiri hiyo ni hali ya kawaida tu, labda kama inazidi sana kuwa akila anatapika, kama hivyo. Kama anakula kidogo na kukataa, basii mpe chakula au maziwa au hicho unachomlisha kila baada ya muda mfupi

Mama Jeremiah said...

Kama afya yake ni nzuri. Nadhani chakula anachokula kina tosha mwili wake.
Ninakushauri hicho kidogo anachokula hakikisha kina virutubisho vyote muhimu. Usijaribu kumuongezea sukari au vitu vitamu tamu ili ale. Kufanya hivyo sio kitu kizuri kwa mtoto.

Anonymous said...

Wangu mie ana miaka mitano sasa. Kula bila kutishana na kushikiana fimbo basi hakuliki! Nimejaribu kila njia. Sasa ivi nimeacha. najitahidi kumpa kila baada ya muda mfupi.