Sunday, July 11

World Cup Final: Xchyler anashangilia Uholanzi!!!

Leo ni fainali ya Kombe la Dunia...Spain na Netherlands aka Holland aka Uholanzi....
Xchyler anashangilia timu ya Uholanzi...sababu kaazima jina lake toka huko kwa wa-Dutch ...anajua aunt Upendo Hartsuiker yuko naye timu moja, maana naye jina lake la mwisho ndio mulemule!!!!

Mdau X ana VUVUZELA lake la ukweliiiiiiii...Babu alifanya kweli kabla hata mashindano hayajaanza, ila mdau hawezi kulipuliza, maana kupuliza vuvuzela kunahitaji pumzi, mi mwenyewe ma'mtu kupuliza mtihani!

X ashanunuliwa mipira minne, (miwili kwa bibi, miwili kwa mama)  maana akasikia KENAKOOO  afu asipouona mpira wake kilio!!!  hilo neno pia kalishika sana...kwa msio fatilia sana maana yake ni "It's time-- Muda umefika" 

X amejifunza kupiga mpira vizuriii, anatumia mguu wa kushoto na kila akipiga ni GOOOOOAL! hata kama ni kwenye kabati!

****
Kombe la dunia ndio linaishia, nitumie vituko vya mdau/wadau wakati wa kombe hili ilikuaje, kajifunza nini kwa mwezi huu wote?

3 comments:

Anonymous said...

Mdau X kanifurahisha sana. Mpira hata ugonge kabati ye kwake ni goo tu, mie mdau wangu ana one year na 5months nimerudi siku hiyo nikakuta amechukua nyanya kwa basket anapiga mpira, du ikabidi nifanye faster kununua mpira maana ye chochote ni kupiga teke.

Pole X kwa kukosa kombe. try next tym

Anonymous said...

Mr X. iyo vuvuzela mi inaniacha hoi kweli, naona umeshajua ata kuipuliza.

Jiang said...

jamani pweza mbaya...timu zangu zote zimetolewa kwa ajili yake!!!apikwe supu tu yaishe!
@Mdau wa kwanza...hoyo mdau ana akili sana, maana ana-improvise! kama hamna mpira kitu chochot cha duara ni mpira!
@Mdau wa pili...anaidumbukiza mdomoni, afu yeye ndio anatoa sauti, sio vuvuzela!