Sunday, August 1

Maziwa ya mwanzo- Colostrum

Unakumbuka maziwa yaliyotoka mwanzo kabisa, kwa kiingereza yaniatwa colostrum. Ni meupee, kwani bado hayajakomaa. Uliyafanya nini? Kama uliyamwaga, au ulikamulia chini, basi umemkosesha mwanao virutubisho muhimu sana, tena vya bureee!
Kuna mila zingine huwa zinamwaga maziwa hayo...kosa kubwa sana, kwani hayo maziwa yana virutubisho vya kumkinga mwanao na magonjwa.
Wataalam wanashauri uanze kumnyonyesha mtoto ndani ya nusu saa baada ya kujifungua, kama hamna mwenye tatizo kati yenu, ili mtoto avipate virutubisho hivyo vya mwanzo pale anapozaliwa tu.
Kunyonyesha sio kazi sana ingawa mwanzo ni mgumu, ila kumbuka, practice makes perfect, hasa ikizingatiwa kuwa kuna wanafunzi wawili hapo, wewe na mtoto. Kazana kumnyonyesha mtoto kila anapohitaji, ndio utakapopata ujuzi zaidi wa jinsi ya kumuweka ili naye anyone vizuri zaidi.
Pia usisite kuuliza watu wenye uzoefu (kama mama, dada rafiki n.k) iwapo utakumbana na kikwazo chochote, isije ikawa kuna kitu hakiendi sana unayamaza tu, uliza usaidiwe.

No comments: