Monday, September 13

Kwa nini tunadanganya watoto?

Hii mada nimetumiwa na mdau, niilete hapa tuijadili!
Mada yangu ni hii, nimegundua watu wa Bongo tunawadanganya sana watoto wadogo?? mfano kazaliwa mtoto mchanga mtoto anaambiwa tumemnunua baby hospitali, au mtoto wa doctor au sababu yoyote ile ambayo haimueleweshi kwamba kichanga hicho kimezaliwa mama, hivi ni kwanini?? au mama ana mimba wanamwambia mtoto nimekula sana, mfano mwingine mama au baba anatoka hamuagi mtoto anamtoroka anasema nikimuaga atalia, mfano mwingine unamdanganya ukila chakula nitakununulia pipi au ahadi zingine kibao ambazo walezi wote mnazijua. 
Swali hivi ni kwa nini tunadanganya watoto?? 
nimebarikiwa kutembelea nchi nyingi zilizoendelea nimekuta watoto wanaambiwa ukweli wakiwa wadogo utakuta mtoto wa wiki anasemeshwa na kuambiwa kila linalooendelea ndani ya nyumba, na kasumba hiyo labda ndio imewajenga watoto wa ulaya na nchi zilizoendelea kuwa wa kweli wa maneno na wawazi wa mambo yao tofauti ya watoto wengi na watu wazima wa bongo wanapenda kusema uuongo uongo na kuficha ficha mambo ambayo hata msingi hayana.

5 comments:

Anonymous said...

kuna mtu aliniambia kuwa mtoto kama unaondoka muage tu na nimekuwa nafanya hivyo toka mwanangu yuko mdogo sana na imenisaidia sana huwa halii kabisa na kama ukimuahidi utamletea kitu ni vizuri kufanya hivyo,usipoaga sasa ndio inakuwa kasheshe.Nikapata ujauzito kabla haujaonekana nikamwambia kuna mdogo wako tumboni baadaye tumbo lilipokuwa kubwa ndio akaamini akasema atatokaje,au anatokea kwenye kitovu mbona kimevimba sana nikamwambia ndio,basi watoto msiwadanganye kwani nilipojifungua tu akaomba kwanza kuona kitovu changu alivyoona kimerudi ndani akaamini kabisa kuwa mtoto anatokea kitovuni so ni vizuri kuwaambia ukweli watoto.Mama Twime

Anonymous said...

Yaani asante sana kwa kuileta hii mada.Jamani mie mwenyewe binafsi sipendi kabsa haka ka style kwa kuwadanganya watoto!!Mie ni mama wa watoto 2,nilivyokuwa na mimba ya mtt wa 2 kwakweli nilimwambia ukweli huyu mtt wa 1 kuwa tumbo kubwa kuna mtt ndani so akawa anapenda sana kuniuliza maswali tena akiamka au akijisikia mwenyewe anauliza mama mtt hajambo na anakiss tumbo langu.Kwa kweli ilikuwa raha na alipunguza maswali sana coz alijua tu tumbo lina nini. Kuna siku aliniuliza sasa mtoto tamtoa lini nataka nicheze nae mama,nikamwambia bado mpaka tumbo liwe kubwa zaidi naenda hosp Doctor akamtoe na siku nilioenda kujifungua na narudi home mwanangu wala hakuwa na hamu na mie alikuwa busy na mtt tena akaanza kuwaambia hata wageni "nampenda Dr kamtoa mama mtt wangu tumboni" hadi shuleni alikuwa anawaambia wenzake na walimu kuwa siku hizi ana mtoto!!Ilinisaidia coz alimpenda mno mpaka leo wote wamekua!!So toka mie siku hizi akimwona mjamzito wala hashangai why tumbo kubwa wala kuuliza kitu coz ameshajua!! Vipo vitu vingi tu tuulizwapo kwakwl tunajitahidi sana mie na mume wangu kusema ukweli. So wazazi wenzangu tujitahidi kuwasaidia watoto wetu kuwaeleza ukweli inapowezekana!!!

Anonymous said...

Mimi naomba wazazi wenzangu kusema ukweli kwa watoto ni kitu kizuri sana tena sio kwenye maswala ya mimba tuu hata maswala mengine ya maisha,tuwaambie watoto ukweli jamani mbona ni kitu rahisi tuu, kwa kweli inabore unakuta mtu mzima anakwambia kitu na anajua fika ni uongo yaani inatia aibu, unajiuliza ni kwa nini unadanganya? lakini ni sababu amekua akidanganywa.

Anonymous said...

Mimi naishi US huku ukidanganya mtoto utaaibika mwenyewe,watoto wa huku wanaambiwa kila kinachoendelea kizuri na kibaya, kwenye kifo ndio usiseme kama doctor amesema umebakiza mwezi kuishi na watoto wanaambiwa mzazi wenu nimebakiza mwezi, tuagane watoto wangu msiogope. Makazini watu wanasema ukweli uongo uongo wa bongo na mimi nimeshauacha siku nyingi, roho yangu nyepesi kabisa

Anonymous said...

Nyie acheni hizo za sijui majuu sijui US. Some uongo kwa watoto wadogo ni jambo zuri, sisi tumelelewa hivyo, wazazi wetu, hali kadhalika mababu na mabibi zetu, huo ndio utamaduni wetu waafrika.msijilinganishe na tamaduni za nje maana hamjui mabaya yaliyopo kwao. Asilimia kubwa ya watoto wa kimarekani wamekuwa abused sexually (kubakwa)wakati wa utoto wao, kama kuna anaebisha na aseme. Je watanzania mko tayari kuingiza watoto kwenye chumba cha kuzaa na kuwaambia waangalie nyuchini wakati watoto wakizaliwa? maana hivyo ndivyo wafanyavyo wamarekani. Jamani tumekulia na hayo mambo ya siri na tumetokea kuwa watu wenye kujiheshimu kuliko hata hao wazungu. Tuzipende mila na desturi zetu.