Wednesday, September 15

Xchyler day one shule


Xchyler, aka X aka Kaila ameanza shule mwanzo wa mwezi huu...tarehe 1 September.


Shule ni St Joseph's Kindegarten School...kama ulisoma Forodhani basi ndio hapo hapo!

(Akirudi home na bibi)
Najua tu mtajiuliza kisa cha kuchelewa kuwapa habari hii, kiukweli siku hiyo tulienda tu kuangalia kama kuna nafasi, maana nilikua nasafiri kesho yake (trh 2) bahati nzuri kukawa na nafasi moja tu, basi hapohapo akavalishwa uniform afu akaongoza darasani...Sister alidhani atatulilia, wapi, ndio kwanza yuko, 'Bye mama, Bya dady'...keshaona wenzake!!!
Pia nilivyosafiri nilisahau kuondoka na memory card, na sikujua niliiacha wapi, imetafutwa muda mrefu kabla haijapatikana last week...ila nikaamua nivute zaidi wape habari hiyo leo....
...sababu, leo, Mr & Mrs Mapunda, tunatimiza miaka mitatu (3) ya ndoa yetu! 
Hivyo, mama na baba Xchyler, tunachukua nafasi hii kuwashukuru wooote waliofanikisha harusi yetu miaka mitatu iliyopita, na kwa wote wanaoendelea kutupa moyo na kutuunga mkono kwenye maisha yetu ya ndoa. Pia tunawashukuru wazazi na ndugu zetu (siblings) kwa mwongozo na mapenzi makubwa kwetu na mwanetu!
Na mwisho tunamshukuru Mungu kwa kutujalia maisha yenye mapenzi na kutujaalia furaha ya maisha yetu, Xchyler, na tunaendelea kuomba azidi kutuzidishia baraka kwenye maisha yetu.
Aksanteni wote.

8 comments:

Anonymous said...

hongera x, mungu akujalie upende shule daima.

Anonymous said...

HONGERA MAMA KAILA, HIVI HIO SHULE HUWA WANATOKA SAA NGAPI MCHANA. ALAFU KAILA ANAMIAKA MINGAPI KWA SASA MPAKA AMEANZA SHULE? KWA UMRI WAKE PALE WANAUANGALIZI MZURI WA KINA BABY KAMA KAILA MANA NATAMANI MWANANGU NAE ASOME HAPO

Anonymous said...

Hongera Kaila kwa kuanza shule. Nami nilisoma hapo Forodhani nursery miaka 30 iliyopita.Naona bado uniform ni the same...

Anonymous said...

Mama XCHYLER, Coment yangu kama Anonymous wa Friday, September 17, 2010 10:10:00 AM GMT+03:00. Tujibu please.

Jiang said...

Anonymous wa Friday, September 17, 2010 10:10:00 AM GMT+03:00
samahani kwa kuchelewa kujibu.
hiyo shule wana shift mbili, ya asubuhi na mchana, wa asubuhi wanatoka saa sita mchana, wanaingia mchana sijui wanatoka saa ngapi.
Kaila ana miaka miwili na miezi mitano, ni mapema kuanza shule, ila imebidi maana mimi sitaluwepo kwa muda mrefu kidogo.
kwa kweli huwa hawapokea mtoto chini ya miaka mitatu (hawataki watoto wanaotumia diapers kabisaaa, kwa ufupi wanataka watoto wanaoongea kidogo na wanaojitegemea kwa kiasi fulani) ila sisi tuliomba kutokana na mazingira na pia ilikua tu kama bahati.

Anonymous said...

Hongera X,
Alivyopendeza na uniform yake utadhani mkaka mkubwa wa 4years, i wish na wangu afike aanze kusoma. Hongera mama X kwa kukuza sasa fanya mchakato mwingine wa mdogo wake (hahaaaa)

Emmy

Jiang said...

Emmy,
atafika tu, na utaenjoy sana kumuona akienda shule, mwanzo unakua huamini kinachotokea...leo naskia kaumia kidogo huko shule, basi ndio story anayoniadidhia kwenye simu, ingawa neno mojamoja, hata haungi sentesi!
huo mchakato wa mdogo wake, na hizo gharama zao, looooh, hata sitaki kufikiria...Mungu akipenda baadae, sio sasa na wote mtajua!

Anonymous said...

hongera baby X kwa kuanza shule, hongera pia kwa mumy X kwa kukuza. X ana miaka mingapi kwani?

Good day!

mumy carol