Sunday, April 8

Hairbandsss za Xy (Shy)

Binti yangu kwenye graduu ya dady...hairband ilimtoajeeeee?
Kuna mdau aliomba kujua zinakopatikana hairbands hizi za watoto ambazo Xy has been rocking kwa kila mtoko wake, iwe kliniki, bichi au kwenda kwa bibi...na si utani zinampendeza mtoto yeyote wa kike, awe na manywele au upara, zinawatoa mchicha tu.
Xy ana design nyingi, za kitai au kiua pembeni kama hii, zenye stones na kadhalika (picha za zingine hata sizioni).
Anyway, mie zote nimenunua au nimepewa na mtu aliyenunua duka linaitwa Zero 2 Twelve, hii nilipewa na mwenye duka baada ya kununua mazagazaga mengine na kuishiwa hela--chezea shoping ya watoto-- wamenihudumia tangu nna kitumbo, kwa kweli nnazimia service zano kichiziii!
Duka hilo kuuubwa lina mavitu ya ukweli ya watoto kuanzia mwaka 0 hadi 12, wa kike na wa kiume...
Duka lipo complex yenye Nyumbani Lounge (kwa Jide), linatazamana na Nyumbani, na huwa liko wazi hadi saa 2 usiku weekdays, so unaweza pita hata ukitoka job jioni...just make sure una hela ya kutosha, usije ukaishiwa kama mie...

No comments: