Tuesday, April 10

Xy's first hair cut

Baada ya kumaliza shooting ya show zake zote, kilichofata kilikua kunyoaaaaa...

Xy alikua na afro siku zote, sionagi sababu za kitaalam za kumnyoa mtoto, najua za kidini za siku 40, ila zaidi ya hiyo sijui nyingine, so huwa siwanyoi wanangu hadi nnapojiskia.

Tatizo afro la Xy ni nywele kuanza kuwa zinajifunga juu, kasheshe kumchana nikataka kumnyoa...loooh, producer wa show ya Fema akasema nisubiri kidooogo wamalize shooting, so walivyomaliza ndio akanyolewa.
Bibi X kama enzi za Xchyler, was there to help me, thank God I have her...I guess I will figure it out nikiwa bibi nikahitajika...
Kazi imekwishwaaaa!
...doesnt she loook cuuuuute!!! 

cruuuuzing!!!

Thank you Bibi X.

4 comments:

Anonymous said...

Habari mama x. Sijapita humu kijijini siku nyingi, hongera sana kwakupata mtoto wa kike. Yaani nimeangalia picha mara kibao sichoki.

Nakutakia kila lakheri katika kumlea binti.

Mama Felista.

Anonymous said...

Hi mama X! Hongera sana mwaya!! Picha ya kwanza nimeipenda sana hilo pozi la kushaangaa kitu!She's cute!!

Mama Emily.

Anonymous said...

Nakapendaga sana haka ka toto kakiwa na bwana ISHI.. nina kababy na mie ka mwaka mmoja na nusu basi akimuona mwenzie anaita toto!!!! ahahahaha ole wako uhamishe channel sasa analiaje!

Jiang nisaidie ninatatizo kidogo mwanangu kachelewa sana kuota meno mpaka sasa ana umri wa mkwa na nusu but ana meno ma4 tu!!
Kwa experience yako is this normal? au nimpeleke kwa dentist afanyiwe check up?

Jiang said...

asanteni jamani kwa kumsifia mwanangu... hapa bichwa kuuubwa!
Anony wa April 17...mi sina jibu la uhakika, as sio dokta, ila kwa experience yangu huwa sio issue, kuna watoto huwa wanachelewa hata hayo manne hawayapati hadi miaka miwili, hasa kama anaafya nzuri na maendeleo mazuri kwenye mambo mengine...ila kama una wacwac sana muone dockta, wa watoto nadhani, si wa meno, akupe amani ya moyoni!