Monday, April 23

Mdau ana cheti cha kuzaliwa?

Cheti cha kuzaliwa ni kitu muhimu sana kwenye maisha yake... uzuri unalipa 3,500 tu kama ukikifuatilia kabla hajasikisha miezi sita!


Hiki ni cha Xyleen kinavyoonekana sasa...
...by the way, kama wewe ni mtoto wa zamani jua tu vyeti vya siku hizi viko updated, ni vizuri na vidogo, sio yake mapande ya karatasi kama enzi zetu!


...Si walikosea wakaandika Male...weeee, binti yangu nilivyomlia timing kumpata afu waniandikie male? Nikabadilisha na kupata kipya in few days!


Maelezo ya jinsi ya kuomba na kupata cheti ingia kwenye website ya RITA HAPA wana kila kitu!

Sorry, kufuatia ushauri wa mdau (asante kwa ushauri na pongezi) nimeamua kuondoa picha za cheti...I hope msomaji unapata maana ya post hii hata kama hamna picha ya cheti. 
Love, Jiang.

2 comments:

Anonymous said...

Umenichekesha, eti binti yako wakakuandikia ni kidume? Ulikuwa makini sana kukikagua unajua muda mwingine mtu unaweza ukaangalia juu juu halafu siku nyingine wakati unahitaji kukitumia ndo linazuka hilo, kwakweli wahusika wawe makini kwa vitu muhimu kama hivyo.

Nilisikia vyeti vitabadirishwa kumbe wameshafanyia kazi? Kinamuonekano mzuri kwakweli sio kama yale magamba yetu.
Hongera na asante kwakutujuza.

Mama Felista.

Anonymous said...

Mdau nakupongeza kwa kuhakikisha mwanao anapata cheti cha kuzaliwa kwa wakati.

Yangu si mengi ila nataka kuweka maelezo sawa....

Gharama ya cheti cha kuzaliwa ni Sh 3,500/= tu kwa mtoto mwenye tangazo. Tangazo hilo hutolewa wakati wa kuzaliwa au ndani ya siku 90 baada ya kuzaliwa. Pia tangazo hilo hutolewa BURE.