Tuesday, April 24

Mimi ni kila kitu!


Mimi ni vitu vingi; mimi ni saa, mpishi, mtumishi, mwalimu, nesi, mlinzi, mpigapicha, mshauri nasaha, mtayarisha sherehe, mwimbaji, mchekeshaji, msaidizi, superhero, dereva, ATM na chochote bosi anachotaka. Kwa huyu bosi, mie ni kila kitu chake!


Kwa kazi hizo zote sina off, wala sick days, wala sikukuu (tena hizo ndo natakiwa sana na bosi). Nafanya kazi usiku na mchana. Niko on call 24/7 kwa maisha yangu yote na wala silalamiki hata siku moja! Nampenda bosi wangu kuliko chochote, na … malipo yangu huwa sio check, wala siwezi kuyakuta kwenye account yangu a benki yeyote.


..niko na mabosi wangu...

Na hii ndio kazi nnayoithamini kuliko kazi nyingine… kuwa Mama!

2 comments:

Anonymous said...

hongera mama x2, mie nimependa viti vyako, ama kweli ni ubunifu ulioje...mama moureen.

Anonymous said...

Mama X sema uko na mabosi wako bwana we, mbona unatenga mmoja, You have two bosses.
Mama JJ(Angela)