Wednesday, April 25

Mlipuko wa ugonjwa – Rotavirus

Kuna ugonjwa wa tumbo umeingia kwa watoto age btn 1 to 5yrs and even to 10 yrs na hospital zote hapa hawaujui,watoto 2 wa kike wamefariki wa kwanza, wiki 2 zilizopita at the age of 4 na wa pili ni Issabella, amefariki jana saa 8 mchana at the age of 3, finally ugonjwa umejulikana, unaitwa Rotavirus, nenda kwa google usome na uwaambie wazazi wenzio... 

Hii nimeitoa kwenye FB account ya rafiki yangu Henry Mdimu, nilipogoogle nikakutana na haya…


Rotavirus ni nini?


Huu ni ugonjwa wa kuhara unaoshambulia watoto wa chini ya miaka mitano. Inasemekana karibu watoto wote lazima waupitie ugonjwa huu by the time wanagonga miaka mitano.


Dalili kuu


Mtoto huanza kutapika akifuatiwa na kuharisha sana, pamoja na homa. Hivi vinasababisha mtoto aishiwe maji mwilini, kitu ambacho kinasababisha vifo vingi vinavyohusiana na ugonjwa huo.


Kimbilia hospitali ukiona…
  • Kuharisha zaidi ya mara nne ndani ya muda wa masaa 12.
  • Kutapika
  • Homa
  • Kama mzazi, tumia instinct zako, zikikwambia nenda hospitali usidharau, hotapoteza kitu (hasahasa pesa kidogo) ukienda daktari akakwambia hamna kitu. Just pata picha utakavyojilaumu kwa kuchelewa kwenda hispitali!Unaambukizwaje?


Kama ilivyo kwa magonjwa mengi ya matumbo hasa ya kuhara, uginjwa huu huambukizwa kupitia kula vitu vichafu vinavyoingizwa mdomoni…(haya wenye watoto wanaotambaa na wanaonyonya vidole sijui tufanyeje?). ila pia unaweza kuambukizwa kwa kupitia mfumo wa hewa.


Kinga


Huu ugonjwa una chanjo, ila hii ni kwa wale walio nchi zilizoendelea aka nchi za mbele, hapa kwetu hamna kitu kama hicho. Kwa kuwa unaambukizwa mara nyingi kwa uchafu, tujitahidi kuhakikisha watoto hawaweki vitu vichafu mdomoni, wananawa mikono kabla ya kula na baada ya kwenda maliwatoni, kina dada nao wafanye hivyo hivyo, including kunawa baada ya kumbadilisha mtoto nepi aka diapers aka pampazi!


Tiba


Mara nyingi madaktari watampa dawa za kutibu hao virusi na matibabu ya kawaida ya mgonjwa wa kuhara.
Kwa ufupi ndio haya, kwa uferu nenda HAPA

Madaktari (as mi sio daktari) mnaweza kuongeza comments…ila naomba msiandike majina ya dawa, maana watu tunapenda kwenda kununua kabla hata daktari hajasema ni nini…

TAHADHARI
By the way, usikimbilie kununua dawa kabla hujamwona daktari, dawa za bakteria hazitibu virusi na vise versa!

4 comments:

Jiang said...

Hii ni comment ya facebook kutoka kwa mdogo wangu Sima, ambaye ni doctor, anasema;
Thanks hii!please shughulikia hii kwa wahusika ili watoe tamko halali la kuwaondoa wamama kwenye wasiwasi maana taarifa niliyoiona inamaswali mengi bado!na case zilizoripotiwa inawezekana ni rotavirus au sio pia sio na mi nasaidia kufuatilia.
8 minutes ago via mobile · Like

Anonymous said...

Watoto wapewe maji mengi ya kunywa ili kupunguza dehydration. Na maji yenyewe yachemshwe kuua vijidudu.

Lulu Kilonzo said...

Mungu wangu Jiang!!! Umenitisha nimeogopa sana............!!! Mwisho wa siku ni Mungu tu atakayetulindia watoto wetu. Ugonjwa huu unasababishwa na nini? Kinga? Tiba? vyote hivi ni maswali yanagonga kichwa changu ngoja kwanza nigoogle then labda nitatulia. Nimeona kwa Shamim yule mtoto Isabella yaani nimeogopa na kusikitika sana. RIP little Angel (Isabella)

Anonymous said...

thx a lot