Wednesday, June 13

Asanteni wote mliochangia, Rukia anaendelea vizuri...
Mnakumbuka yule mdau Rukia aliyeungua kwa maji ya moto aliyehiaji msaada...well habari nilizopata toka Chingaone Blog ni kwamba kwa sasa hali ya vidonda imeanza kuleta matumaini makubwa ukilinganisha na mwanzo.
Vidonda vimeanza kukauka na kupunguza kutoa maji kwa kiasi kikubwa hali inayoleta faraja kwa RUKIA na wazazi wake.


Kwa sasa hali ya mtoto RUKIA inazidi kuimarika na  kuleta matumaini na nuru! tunawashukuru watu wote waliotoa msaada hadi kufikia sasa, Matibabu bado yanaendelea na bado tunahitajika  kwa hali na mali kumsindikiza mtoto huyu katika safari yake ya matibabu. Unaweza kuchangia kiasi chochote kwa ajili ya matibabu, michango inaendelea kupokelewa , wa kwa maelezo zaidi tuandikie chingaone@gmail.com au tuma mchango wako kwa Uncle  Victor Richard  kupitia akaunti ya M- PESA 0755 754494, TIGO 0715 754494.

No comments: