Thursday, June 14

Rukia ametutangulia!


Naandika hapa kwa masikitiko, nimetoka kupokea habari sasa hivi kwamba mdau Rukia aliyekua anauguza vidonda vya kuungua moto amefariki dunia jioni hii.

Taarifa nilizopata jioni hii ni kwamba alikua na malaria, ambapo madaktari wanasema kuwa vidonda vilikuwa vinaendelea vizuri, ila ni malaria aliyokutwa nayo leo mchana ndio imemuondoa.

Mungu ailaze pahali pema peponi roho ya malaika huyu.

Asanteni wote mliojitolea kwa hali na mali kuchangia matibabu yake. 
Asante sana kaka Victor Richard, uliyefanya tulio mbali na mtoto huyu tupate taarifa zake.
Asante sana Akoth Loyce for updates ulizokuwa unanitumia mimi binafsi.

No comments: