Tuesday, June 12

Kuna Dr Massawe mmoja tu mji huu?

Jumatatu hii, yaani jana, kwa mara ya kwanza nilienda kumuona Dr Massawe. Sina haja ya kuelezea kuhusu uzuri wa huyu doctor, kwa kweli nimeridhika na matibabu yake sana, sana, sana na wengi mnajua sifa zake, iwe kwa kuhadithiwa au kuexperience mwenyewe.
Tatizo langu ni ile kuwahi namba kunakotakiwa. Jumapili sisi hatukulala, tulikaa Coco Beach hadi saa sita usiku, ndo tukaenda (anyway, that was extreme, ila tulishaenda saa tisa usiku tukakosa namba, so tuliamua kuto-takechances). Mtu wa pili alifika kwenye saa nane na robo, na mtu wa mwisho alifika saa 10:05!!! Yes, wote waliofika baada ya hayo, ilikua imekula kwao, as walikua washachelewa namba.
Hii yote inatokana na nini? Demand, jamani. Maana mie kila nikiulizia naambiwa hamna kiboko kama Dr Massawe, na kwa kweli ni mzuri, ila 
JE, MJI HUU, HAKUNA DAKTARI WA WATOTO MWINGINE MZURI KAMA DR MASSAWE?
Jamani tusaidiane, niandikie hapa kwenye comment dokta gani mwingine unayemfahamu ambaye ni mzuri kama Massawe, tupe jina, anakopatikana, na exerience yako...ni vistory vya kumpeleka mtoto kila hospitali akashindikana, afu Massawe akakuta ni allergy tu vinavymfanya Massawe awe juu.
Kama story yako ni ndefu sana unaweza kutuma kwanye mamanamwana@gmail.com
Then, nitaweka post nyingine ya kushare kina Massawe wengine wa mji huu, mlionifriend Facebook, huu mjadala ulikua mrefu sana huko, kwa faida ya wengi nimeuhamishia huku!

Naomba ieleweke kwamba nia ya hii post sio kumpunguzia Massawe wateja, am sure anamore than he needs, ila ni kutupa wazazi options ya kutolazimika kukesha (pia am sure hapendi tukeshe ndio maana kuna tangazo la kutokesha pale mlangoni kwake) kwa kujua madaktari wengine wa watoto wazuri ambao wanaweza kuwatibu wanetu tukaridhika. 

8 comments:

Anonymous said...

Kuna Dr Dulla pale pale kwa Massawe, ni mzuri mno, kuna Dr Namala yeye anapatikana muhimbili ila ana clinic upanga pia, kuna prof Kareem yuko upanga kwake pia kuna foleni na huwezi ku re great kupanga foleni akishamuona mwanae.. kuna dr Hameer kariakoo, kwake kuna foleni hujawahi ona nilienda sa 3 nikapewa namba 99 sikuweza kusubiri kwa kweli maana mtoto alikua anaumwa sana ila wanasema pia ni mzuri

Anonymous said...

Kuna Dr. Kaja yuko M/Nyamala Komakoma ni mzuri sana kwa tiba na ushauri mzuri. Ndo anayemtibu mwanangu sasa ana miaka 4.

mama wawil said...

mimi kwa upande wangu huwa naenda kwa dr hassanal kwa kweli kwa wanangu naona huwa wakienda pale wanapata tiba tosha kwani huwa nakwenda hosp zingine mtoto aendelea kuumwa ila nikienda pale anapata ahueni

Anonymous said...

Kuna Doctor Hasanali, Mtendeni Clinic, Karibu na Mtendeni Primary school maeneo Kisutu. au anapatikana Trauma Centre masaki. Naye ni Mzuri hakuna foleni za kutisha na dawa anatoa yeye mwenyewe. Pole ametusaidia sana sie na watoto wetu kwa muda mrefu. Mwanangu ana miaka 6 sasa na no Dr. wake.Mjaribu

Anonymous said...

Nilipoelezwa kuhusu dr Massawe miaka mitano iliyopita, nikaanza mchakato wa kwenda kumwona. Wakati huo alikuwa bado anachukua wagonjwa ishirini. Ngoma ilikuwa nzito zaidi maana ilikuwa unawahi pale wakati nyota bado ziko angani, 'mnajigawia' namba kiujanjaujanja maana ilikuwa kama vile hairuhisiwi, namba rasmi zilikuwa zinatolewa dirishani mchana unapokwenda kuandikisha, hivyo hata kama ulidamka saa kumi, akikutangulia mtu kwenye foleni ya dirishani saa nane umeumia!
Haikuwa rahisi kwa aliyedamkia pale kuwahi foleni ya saa nane mchana maana ilikuwa huwezi kufungua/kuandikisha faili na kupewa namba hadi uje na huyo mtoto mwenyewe wamwandikishe akiwepo! sasa kama wewe umedamka, mtoto utadamka naye kisha ukae pale hadi saa nane uandikishe kisha uendelee kukaa mpaka saa 11 daktari atakapokuja?
Ilikuwa haiwezekani, hivyo kilichobaki ilikuwa ni kutumia ubabe, ikawa ujanja ni kupata, sio kuwahi! Kwa ufupi ni mwendo wa mwenye nguvu mpishe, maana niliwahi kushuhudia laivu mibaba miwili ikitwangana makonde hadharani, mwingine akidai alikuwa mtu wa pili kufika saa kumi alfajiri, mwenzake akadai yeye ni wa kwanza dirishani! Nesi kuona hivyo alisepa, akaacha watwangane makonde kwanza, kisha atakayeamua kumvulia kofia mwenzake atambae zake, aliyevuliwa kofia apate hiyo namba! Hali ilikuwa mbaya na ndipo nilipojiuliza swali kama unalojiuliza wewe mama x, 'hivi hakuna daktari mwingine mzuri kama dr massawe mji huu?"
Niliifukuzia namba kwa siku tatu bila mafanikio, hapo ndipo niliposhauriwa na manesi wa pale kwamba nimwone Dulla. Huyu ni daktari mwingine wa palepale, ambaye ametajwa na anony aliyechangia mwanzo! Nikakubali shingo upande, nikapewa kijinamba cha mkiani, nikavuta subira nikamwona. Dullah ni mzuri, alimtazama mwanangu kwa muda wa kutosha, hakumwandikia dawa yoyote, na naamini hata Massawe asingefanya jambo tofauti na hilo.
Nilirudi nyumbani na amani na mwanangu baada ya muda alikaa fresh kama alivyoniambia Dullah na kuanzia wakati huo sikuhangaika sana na Massawe mpaka hivi majuzi nilipopata mtoto njiti ndipo nikaanza kusota naye tena kwakuwa naambiwa ni mtaalam sana wa njiti pale Muhimbili na kwakuwa sikujigungulia pale nililazimika kumsaka!
Madaktari wako wengi kama alivyosema mdau aliyetangulia, ila imani inatuponza tunakosa usingizi bila sababu!
Pale kwa Dr Massawe hata ukimwona general practitioner ni sawa, kwani ingawa sio maspecialist wa watoto lakini wana uzoefu kazini kwani kila siku wanashughulika na watoto na wanakumbana na kesi mbalimbali, ya kwako haiwezi kuwa ya kwanza! Pia dawa wanazotumia ni zilezile zinazopatikana pale, maabara ni ileile na cha muhimu katika tiba ni ugonjwa ujulikane, hivyo kama hospitali unaamini maabara zake basi unaweza ukatibiwa na daktari yeyote hapo. Madaktari wengine wa pale wako tangu asubuhi mpaka saa nane na wala hawana foleni kiviile, unawaona kiulaiiiini!
Enewei, email yangu ni ndefu sana, wadau mtanisamehe kwa kuwachosha kwa ‘mkeka’ huu, ila nia yangu ni njema, tupate kueleweshana, tusijichoshe na kujikosesha usingizi. Naomba nami nieleweke kwamba sina nia ya kumharibia Dr Massawe, ni daktari mzuri sana, tena sana, huwezi kujutia kumpangia foleni lakini madaktari wengine pale, Dullah na wenzake they are almost equally good, dawa za pale ni nzuri na maabara yao imekaa fres. Unless una a very very very special case, otherwise kamwone yeyote.

Kila la kheri katika malezi wadau

Mama Jj

Anonymous said...

Kuna daktari mwingine anaitwa DR.YOHANA,ni Dr wa watoto na clinic yake iko pale Elia Complex Opposite na chuo cha CBE,jamani this DR is very good aisee...na ana dawa nzuri mno,kinachonivutia kwake ni kwamba anamcheki mtoto vizuri mnooo na pia he takes his time kukuelewesha kinachomsumbua mtoto na kukushauri pia...mjarubuni hamtajutia na wala hana foleni za kutisha

Anonymous said...

Ni kweli Dr Yohana hutajuta ukimwona, na clinic yake ni full watoto, mimi sipeleki watoto wangu kwingine zaidi ya kwake, he is a loving Dr na wala hana foleni, foleni yake ni ya kawaida mno, huwa nashangaa sana kwa jinsi alivyo mzuri mbona hana foleni sana; nadhani watu hamjui sana, lkn wadau jaribu, hutajuta, uzuri wa Dr massawe yeye pia yupo muhimbili kwa hiyo mtoto kama ana complication sana huwa anakuambia uende muhimbili ili awe anakuhudumia karibu na vipimo vikubwa zaidi

Anonymous said...

Dr Yohana jamani ni mzuri saaaaana Mtoto wangu alikuwa anaharisha na kutaapika tu bila kufunga alihangaika nae na akapona ila yupo makini na anafuatilia sana na pia anakupa ushauri wa chakula ni wewe tu ujue jinsi ya kutaka akusaidie anapenda sana watoto na watoto wakiwa kwake wanajiona kama wapo sehemu ya kuchezea na sio hospt....