Tuesday, June 5

Mdau anahitaji msaada haraka!
Mtoto RUKIA ABDALHA ni mtoto wa miaka miwili anayeishi RUANGWA (LUGALO) mkoani LINDI alipata ajali ya kuungua na  maji ya moto, ameshawahi kutibiwa katika  hospitali ya wilaya RUANGWA ambako alipatiwa huduma ya kwanza na kushauriwa aende katika hospital za NDANDA, NYANGAO au MUHIMBILI. Wazazi wa RUKIA hawana uwezo kifedha  na kushindwa kufanya matibabu ya majeraha ya mtoto huyo hadi sasa!  

Kwa sasa mtoto RUKIA anatibiwa  na dawa za kienyeji huko nyumbani kwao, hali ya vidonda sio mzuri inazidi kuwa mbaya siku hadi siku! Vidonda vinazidi kuchimba mwili na  kusababisha harufu kali na mateso kwa mtoto huyu. Kwa niaba ya familia tunaomba msaada wa hali na mali kwa mtoto huyu, tunaomba msaada wa  aina yoyote utaoleta mabadiliko kwa mtoto huyu.  

Kutoa ni moyo, tuma hata 1,000/- tu maana haba na haba hujaza kibaba. 
Kama wazazi, tunaojua uchungu wa mtoto kuumwa tujitolee kutuma pesa kumsaidia mdau huyu aliye kwenye mateso makubwa. Tuma pesa kwa Victor Richard M-pesa 0755 754494/tigo pesa 0715 754494.

Hii habari imeripotiwa blog mbalimbali leo, ila picha zaidi unaweza kupata HAPA.

No comments: