Monday, August 27

Eti kuna nini wodi ya kina mama Mt Meru hosp?


Nimeikuta inbox hii:

Leo nimesikia tena habari ya kusikitisha juu ya ama uzembe au kiwango cha chini cha upasuaji wa wazazi hospitali ya Mt Meru Arusha. Mimi kama mtu mmoja nina ndugu wawili waliojifungua kwa operesheni mwezi huu na zote mbili kufumuka na kurudiwa mara mbili. Wa kwanza alijifungua mtoto kwa upasuaji lakini baada ya wiki imefumuka hadi kurudishwa hospitali. Huyo wa pili kajifungua wiki na leo amerudishwa maana nyuzi zimefumuka tena. Ndugu aliyekuwa ananipa taarifa akawa anasema ni shetani.

Nikamwambia siyo kweli kwa sababu mbona hospitali za binafsi hazifumuki? Kwanini iwe Mt Meru tu? Ndio nikasema ama ni uzembe au kukosekana kwa wataalam wa upasuaji. Hebu watu wa Arusha mtusaidie kufuatilia kujua kulikoni. 

Jamani naomba tusaidiani kujua kunani hospitali ya Mt Meru?

Wadau wa pande hizo, hebu tupeni majibu...

No comments: