Friday, August 24

Tuwachunge watoto na magari

Nimetoka kuzika mtoto wa jirani, yaani ni jirani ambaye nyumba zimegeukiana, akiwa anaanika nguo au nikiwa naanika nguo tunaonana, na pia tuko Jumuiya moja.
Mtoto ana miaka miwili plus, kwa kweli imenisikitisha sana kifo chake. 
Amegongwa na gari, nje kwao jana asubuhi...dereva wala hakuwa anaenda kasi.
Dereva ni mkazi wa hapohapo mtaani, akawa ametoka kwake amesimama anasalimiana na mtu, mtoto katoka ndani, akasimama sijui karibu na tairi, bila mtu kumuona dereva akaondoa gari, akamkanyaga mtoto.
Nilishtuka sana nilipopigiwa simu kuambiwa jana, ni jambo ambalo lingemkuta mtoto yeyote, hata Kaila wangu (X mkubwa) maana anachezaga mitaa hiyohiyo...Jana naingia tu home, Kaila ananiadithia, "mdogo wake Eric kagongwa na gari", though hakuona ajali yenyewe... Huko kwenye mazishi, Eric mwenyewe, ana umri kama wa Kaila, wala haelewi kinachoendelea, ameweka shada na kutupia mchanga bila kuelewa kwamba hatakuja kumuona mdogo wake tena.
Tuwaombee na kuwalinda sana malaika wetu.
RIP Wilson Temba, wazazi Mungu awape nguvu kupita kipindi hiki.

1 comment:

Anonymous said...

Pole sana mama X na familia ya marehem mungu amuweke mahali pema peponi.

Nimesikitishwa sana na hii taarifa kwani kama ulivyosema inaweza ikamkuta mtoto yeyote. Namuombea hata huyo dereva kama ulivyosema anaishi jirani na maeneo hayo, wote wapo katika wakati mgumu.

Nikisikia kifo tena na watoto wadogo nasikitishwa sana. Mama Eric na familia mungu awape nguvu yeye aliye juu ndo muweza wa yote.

POLENI SANA.

Mama Felista.