Friday, August 31

Unaondoka analia? Ufanyeje?

Ni kweli kuwa inaumiza kuona mwanao analia. Tena analia akiwa anakulilia wewe.
Inatokea mara nyingi ukiwa unajiandaa kutoka aidha kwa kwenda job au sehemu
nyingine. Ukiwa unajiandaa anakuangalia anakufurahia hadi unamaliza.
Unapobeba mkoba tu kilio kinaanza. Ndio kinaanza coz anajua muda wa kuachwa umewadia.

Ufanyeje unapoona hali hii?


  • Inabidi wazazi tukubaliane na ukweli kuwa hata alie apasuke ni lazima na yatupasa tutoke. Hakuna jinsi so  ni lazima aachwe.
  •  Sasa basi, we ondoka huku  anakuona na analia kwa nguvuuu ( Inauma lakini) coz utaondoka baada  ya muda kupita atanyamaza tu.
  •  Kama inawezekana pale pale anapolia, mfate mkiss muage. Mwambie: Mama anaenda kazini,  atarudi baadaye.
  •  Mwanzoni itakuwa ngumu lakini siku zinapozidi kwenda yeye mwenyewe ataacha kwani atagundua kuwa hata akilia machozi ya damu wewe bado utaondoka tu. 
NB: Ni vizuri kujijengea tabia ya kufanya hivi pindi watoto wanapopata akili ya kutambua kwani mtoto   atakuwa anakuamini siku zote. Ukimtoroka haitasaidia tena atakapokuwa mkubwa inampotezea uaminifu kwako kwani akili za watoto zinakusanya mambo.

2 comments:

mama wawili said...

muda mwingine analia si kwa sababu mama unaondoka ila ana ujumbe ambao wazazi huwa hatuuelewi inaweza tokea akawa ananyanyaswa au anateswa so analia kukuambia japo hajui kusema . so tuwe makini kwa options zote

Anonymous said...

nadhani ni kweli inauma sana,ingawa bado sijapata uzoefu kwa hilo, hapa nina ujauzito wa miezi kadhaa lakini sipati picha siku nitakayoanza kumwacha kwa mara ya kanza. ingawa atakuwa bado mdogo hatambui kitu lakini kama mama ntaumia.