Friday, September 7

Nasafiri, nna mtoto ananyonya, nifanyeje?


Mdau anaomba msaada....

Mi ni mama wa watoto wawili, Fetty (6) na Faysal (1 yr). nafanya kazi kwenye NGO moja inajihusisha na advocacy works. sasa natakiwa kusafiri nje ya mkoa kwa takribani siku 45. huyu mdogo bado ananyonya na huko ninapoenda ni rural areas and nitakuwa nahama hama wilaya moja kwenda ingine  ndani ya kipindi hicho. 

So what troubles me ni kuhusu mtoto huyu mdogo (Faysal): kumuacha nyumbani kwa kipindi hicho chote wakaati bado ananyonya ama kwenda naye. 
Je, wadau hebu nishaurini nifanyeje, maana nikiwaga na trip za upcountry ila mjini namchukua but sahivi ni upcountry -rural. Naogopa usalama wake kusafiri hadi huko, sehemu ya kufikia (malazi) na hata hali za hewa huko tuendako. 

Nisaidieni mawazo wamama 

Mamake Faysal

4 comments:

Anonymous said...

Habari mama Faysal, pole na majukumu.

Wazo langu mimi ungemchukua dada wa kumlea pindi uwapo kazini kama unaye. Lakini shida ya usumbufu katika usafiri bado unayo haikwepeki kwani atachoka na hata dada pia. Jingine ungeweza kumuachisha lakini hii kama haukuwa na mpango kwakweli inauma sana hautakuwa na raha ya kazi.

Shauriana na baba mtoto umsikie naye ana lipi.

Pole sana mama mwenzangu najua unaumia sana kama huku pangilia haya yote.

Anonymous said...

Duh pole sana mama, mimi pia ilinitokea kipindi mwanangu alikuwa na mwaka nikapata safari nje ya nchi, kwa kweli nilichukua uamuzi mgumu sana ikabidi nimuachishe.
Sasa yuko poa sana tu na ana 2yrs. aliendelea kunywa maziwa ya ng'ombe na uji wala hakupungua uzito na ana afya njema mpaka leo.

mama Glory said...

kusafiri naye utajitafutia matatizo mengine, kwa sababu mtoto bado mdogo pia kubadili hali ya hewa ni tatizo lingine, cha muhimu zingatia haya mwachishe au kataa hiyo safari so chagua moja mtoto na kazi, lakini mimi nakushauri kama utaamua kumwachisha na kusafiri tafuta mtu wa karibu wa kukuangalizia mtoto, eidha mama yako au mdogo wako, lakini usimwache na dada tu.

Ysha said...

Asanteni wamama kwa maoni yenu.
Nimeshauriana na baba na bibi yake kuwa nimuache (hiyo inamaanisha nimuachishe nyonyo). Hivyo atabakia na wadogo zangu wawili wakisaidiwa na bibi yake (mzaa baba kwani wangu keshatangulia mbele za haki). Yeye hakai mbali nasi.
Kweli ni uamuzi mgumu but cna jinsi as nilishazikacha sana trips kwa kigezo cha mtoto mdogo but hii naona sitoeleweka.

Naamini mungu atamlinda na ntawasisitiza antu zake wamuangalie vizuri, pia ntakuwa nawakumbusha kwa simu.

Nawapenda sana wote mlionishauri.

Mama Faysal