Friday, October 12

Siku ya Mtoto wa Kike

Kwa mara ya kwanza leo, Umoja wa mataifa unaadhimisha siku ya mtoto wa kike duniani.
Moja ya madhumini makuu ya siku hii ni kutadhmini changamoto zinazomkabili mtoto wa kike.

Huyu anaitwa Asia, ana miaka 14, akimuogesha binti yake mchanga, huku pembeni mwanae wa kwanza mwenye miaka miwili akiwa anacheza...picha zaidi za ndoa za utotoni BOFYA HAPA.
Kauli mbiu ya mwaka huu ni Ukomeshaji wa Ndoa za Utotoni... sijui kama serikali yetu inaliona hili, ila sheria kuruhusu mtoto wa kike mwenye miaka 14 kuolewa kwa ridhaa ya wazazi ni uonevu, udhalilishaji, unyanyasaji na ukiukaji wa haki za msingi za mtoto, coz seriously mtu wa miaka 14 is just a child! awe msichana au mvulana!
Mtu ambaye sheria haiamini kwamba ana uwezo wa kupigia kura mwenyekiti wake wa serikari ya mtaa/kijiji u kingozi mwingine yeyote wa serikali, inawezekana vipi akaaminika kuwa na uwezo wa kubeba majukumu ya umama??? Tafakari...

1 comment:

Anonymous said...

uko kimya jiang? ni aje coz i rly lyk ur blog mamii usitunyime raha wadau wako!