Monday, November 19

Ushatuma picha za mdau kwenye shindano?


Si unajua kuwa watengenezaji wa bidhaa bora za watoto za Bebi, ChemiCotex Industries Limited wanawaletea shindano la Photogenic Baby au Picha Nzuri ya Mtoto...sasa unangojea nini kutuma picha?

So, Mama, Baba, Anko, Anti, Bibi na Babu, si una ka-cute hapo home, huu ndio wakati wake wa kunufaika na zile sifa unazopata kuambiwa "baby mzuriii/she is sooooo sweeeet/ jamani mcuuuute/Jamani kazuuuuuri haka katoto" maana atapewa zawadi za bidhaa mbalimbali toka Bebi.

Lengo la shindano hili ni kuwaleta wazazi pamoja na watoto wao wenye umri kati ya miezi 0 hadi miezi 18 (mwaka na nusu). 
Shindano hili ni kwa ajili ya watoto walio ndani ya Tanzania pekee na litaendeshwa kuanzia tarehe 1Novemba hadi 30 Novemba tu, so bado hujachelewa.

Piga au pata picha nzuri ya mwanao kisha tuma hiyo picha kwa njia mojawapo:

Tuma barua pepe kwenda photobebi@gmail.com 
AU
peleka TSN Supermarket, Shoprite na maduka shiriki.
Bado wiki mbili tu!!!

No comments: