Friday, January 11

Mjue zaidi Carine aka SweetieUnaweza kumuita Carine hili ni jina la ubatizo na la nyumbani anaitwa Sweetie

Mimi ni mama yake mzazi Carine, ni mtoto wangu wa kwanza katika uzao wangu na kwa sasa Carine ana miaka mitatu (3).

Carine alizaliwa katika mkoa wa Tanga hospitali ya Bombo, alipotimiza miaka miwili bibi yake mzaa mama alimchukuwa na kwenda kuishi naye mkoani Kilimanjaro. Miezi miwili iliyopita nilimchukuwa na kukaa naye ili kuweza kugundua mwanangu anapenda nini na niligundua anapenda sana michezo kama kuogelea, kukimbia n.k. pia anatumia mkono wa kushoto. Carine anasema "mimi napenda sana mazoezi kama kukimbia"


Carine bado hajaanza shule lakini najipanga ikiwezekana mwezi wa sita anaweza kuanza chekechea. Nampenda sana mwanangu. 

Mbaya zaidi Carine analelewa na mama tuu au naweza kusema anapata mapenzi ya mama tuu maana baba yake Mr. Jeremiah alifariki mwaka 30/06/2010 Carine akiwa na miezi 5. Hata hivyo namshukuru MUNGU sana.


By Esperance aka Mama Carine.

3 comments:

Anonymous said...

Pole dada Mungu atakukuzia mwanao katika kimo na maarifa, usiumie kulea peke yako, yote mipango ya Mungu

Mama Abigail said...

Carine ni mcuuteee hasa.Muombe Mungu mpenzi,hatakuacha peke yako katika malezi ya malaika huyu.Nakutakia malezi mema

Anonymous said...

Mama carine hongera kwakupata mtoto mzuri na mwenye afya nzuri. Nina mdogo wangu anaitwa jina kama lako tofauti yake ni ndogo sana (Esperansia)sijawahi kulisikia ndo hapa leo.

Yote mwachie mungu, mtoto anaweza akakuzwa na baba na mama halafu baba akawa kero tupu.Hiyo yote nimitihani ya dunia.

Muendeleze mtoto kwa hivyo vipaji vyake na mungu atamsaidia.

Mama Felista.