Showing posts with label Jina. Show all posts
Showing posts with label Jina. Show all posts

Monday, June 1

Valencia

Valencia, breath taking B-E-A-U-T-Y.....
*****


Hii ndio historia ya jina la mtoto Valencia, kama inavyosimuliwa na mama yake, Lulu Kilonzo, "Nikiwa mjamzito, nilikuwa nafikiria ni jina gain nimpe mtoto wangu kwani nilishajua kuwa nina kabinti tumboni. Kwa kweli nilikuwa ninataka jina litakalo kuwa na maana nzuri na pia litakalo unganisha majina yote yaliyopo kwenye familia yangu yaani baba, mimi na watoto.
Nikapata jina la Vanesa, amablo nililipenda ukizingalia kuwa ninampenda sana mwanamuziki Vanesa (Save the best for last) na mcheza tennis Sasa ilikuwa nijifungue January 2008 duh!! Basi nikapitiliza zaidi ya week 42 mpaka dr wangu Shafiq akaamua kunifanyia induction mwezi February huo sasa, baada ya kujifungua ndo nikagundua kuwa ilikuwa ni Feb 14 2008 yaani Valentine’s day!!!!
Ikabidi hapo hapo tukubaliane na babake kuwa mtoto tumuite Valencia yaani ni Muunganiko wa majina ya babake, mimi na nduguze vale lakini pia tuliheshimu “Valentine” The meaning of the name Valencia is Strength, Health.
*****
Sina la kuongezea juu ya hilo jina, lakini duh, huyu mtoto mzuri jamani....mi hata nashindwa kuongea.

Thursday, May 28

Jina la Hosam Hassan


Mdau Mama Hosam Shadida anasimulia kuhusu jina la mwanae mpanzi Hosam Hassan:

"Mwaka 1993 nilikuwa nasoma gazeti sehemu ya michezo nikaona jina la mchezaji wa Misri aitwae Hosam Hassan,nikalipenda sana jina hilo jinsi lilivyofuatana na linavyotamkika,nikasema nikimpata mume aitwae Hassan nitamwita na mimi mtoto wangu Hosam.
"Bahati nzuri ndoto yangu ikawa ni ya kweli namshukuru Mungu,nikampata,sikuwa nikichagua jina wala ni bahati yangu,tulifunga ndoa 17/11/2006,niliposhika ujauzito nikamuelezea kesi yangu nae akawa upande wangu, tarehe 3/08/2007 nikajifungua baby boy ndio babaake akamwita hilo jina.

"Kutamkwa kwake ni "HUSAAM" ila kuandikwa inaweza kuandikwa Hossam,Husam,Hosam, au kwa kirefu chake ni "Husaamudeen" au "Husam-Al-Deen"Maana yake ni "SWORD" au ukimalizia Husaamudeen inakuwa na maana ya "The sword of the faith""

*****

Kwa kuongezea tu wadau ni umhimu sana kuzingatia muendano na jina la mwisho, unapochagua jina la kwanza la mwanao, mi nimesoma na mtu anaitwa Tukae Msosi, si mnaona lilivyo zuri, yani siwezi kusahau jina lake, hata nikisahau sura.

Monday, May 25

Jina La Xchyler

Watu wengi wamekua wakiniuliza matamshi, maana, asili na nilifikiria nini hadi nikampa mwanangu jina la Xchyler.
Ili kuondoa maswali mengi na kuwaridhisha wadau, nimeona tu subiri nijibu yooote kwa pamoja.
Kuna njia nyingi za kupata majina ya watoto, ila hilo ntaliongelea siku nyingine, kwa Xchyler, kabla sijapata ujauzito, nilifikiria nikija kupata mtoto ntamwita lenye maana ya Malaika, ila kwa lugha isiyozoeleka kabisa, ili liwe la kipekee. Na focus yangu kubwa ilikua ni kupata jina la kipekee (unique), as mimi nina jina la kipekee, kwa hapa bongo (China jina langu ni kama Amina Neema au Asha, maana kila mtu analo) hivyo najua faida na hasara za kuwa na jina la kipekee.
Basi, baada ya kuwa mjamzito nikatafuta sana malaika kwa lugha tofauti tofauti, ila zote sikuzipenda, baba yake akasema, tutafute tu unique names, zenye maana yeyote nzuri. Akatafuta, na mimi nikatafuta, tukapata jumla ya majina kama 20 tuliyoyapenda, 14 ya kike, 6 ya kiume, na Xchyler ndio lilikua pekee linaloweza kutumika kote.
Kwa mtoto wa kike mimi nilipenda jina flan hivi, Qiana, la wamarekani wale wa asili (Red Indians), ila lilimtatiza sana baba yake akidai kuwa wabongo kama kawaida yao kupenda urahisi watakua wanamkatisha Ana, na yeye hataki jina common kwa mwanae.
Yeye tangu mwanzo moyo wake wote kwenye Xchyler, tena akawa anaona urahisi maana hata akiwa wa kike au wa kiume hatutabadilisha, ila mimi niliona ni refu sana, ukizingatia jina kamili ni Xchyler Mapunda, ila baba yake akasema mbona na yeye ni refu, Sixtus Mapunda.
Alijitahidi kunishawishi, hadi baadae nikaona ni zuri, na kiukweli nalipenda sana, I cant imagine mwanangu huyu aitwe jina lingine, naona kama linamfit sana.
Asili: Hili jina linatoka kwa wa-Dutch, nchi inayoitwa Holand/Netherlands (hii nchi timu yake inavaaga jezi za orange, niliizimia tangu nasoma Jangwani).
Maana: Msomi, mwanazuoni (scholar/Intelectual)
Matamshi: Xchyler linatamkwa kama unavyoisoma skyler, na kuna watu wanaliandika hivyo.
Kukatisha: Mimi napenda kuliandika X, na watu wengi wanaliandika hivyo ili wasikosee, ila kumwita napenda kumwita 'kailer' ,na mwenyewe anaelewa. Watu wengi, waliokua siku nyingi wanatafuta sababu ili wasitamke jina langu, maana nalo mtihani, wananiita Mama X, na napenda kuitwa hivyo pia.
Spelling zingine: Skyler, Schyler, Schylar, Skylor, Skyller, Skuyler, Schuyler
*****
Nadhani hadi hapo hakutakua na maswali tena kuhusu jina la Xchyler.
Najua kila jina lina story nyuma yake, niandikie kuhusu jina la mwanao, ambatanisha na picha ya mtoto, tu-share na wadau, maana wengine bado wanatafuta majina.