Thursday, January 30
Tuesday, August 13
Karibu Suzan
Mdau mpya ameingia mjini,anaitwa Suzan hapa akiwa na siku nne duniani.nampenda sana baby suzan namtakia maisha marefu.
Mama Suzan.
***
Mama na Mwana inakukaribisha duniani na kwenye playground yetu hii hapa Suzan.
Thursday, June 13
Birthday party ya Hoka ilinoga haswa!
Birthday girl...beautiful Hoka...
Hoka birthday tarehe 24/5/2013 alisharehekea akiwa na marafiki zake na majirani zake.
..tamtam...
"Namshukuru mungu sana kwa mwanangu kufikisha miaka hiyo mungu azidi kumkuza vema."
Asante mama yake Hoka.
Wednesday, June 5
Mdau mpya in town
Hi watoto wenzangu naitwa warda. Na mpenda mamy saana akurudi kazini nacheka nae huyo akiondoka kwenda kazini na mmiss sana mamy yangu. Penda mimi sana i love you all toto.
Tuesday, May 21
Hi toka kwa Carine
Habari zenu watoto wenzangu naitwa Carine leo niko hivi, muda mrefu sijapita kuwasalimu. tatizo mama ananibania kunipiga picha jamani.
Nawapenda sana rafiki zangu, wasalimie baba na mama zetu huko majumbani.
By Carine
Monday, May 13
Mother's Day card by X -- My first ever!!!
Kadi yangu ya kwanza, ever!!!, ya kunitakia Happy Mother's Day...from my son, Xchyler...so proud of him...and thanks to the teachers for making this happen!
Kaila is a big-boi now...huu mwandiko wake mwenyewe!!
Happy Mother's Day--from Ohio
It's Mother's Day! Aika na Mama yake Cecy Njau wakipozi kwa picha katika kusherekea siku hiyo muhimu duniani huko Columbus, Ohio nchini Marekani...
Monday, May 6
Mlipuko wa Arusha--sasa na malaika huyo amewakosea nini wahusika?
Pamoja na kuwa wahanga wa mlipuko wa Arusha pamoja na watanzania wenzangu hatuelewi sababu wala nia au hata ujumbe aliotaka kuufkisha huyo aliyelip[ua...
Pamoja na kuelewa kwamba alirusha bomu kanisani, that is sehemu ya ibada, katikati ya ibada, akielewa fika kwamba kutakuwa na watu wa rangi, jinsi na umri mbalimbali...
Pamoja na sikitishwa na utokeaji wa tukio hili, na mengineyo yanayofanana na haya (bila kuwa na nia ya kuyaunganisha kana kwamba yamefanywa na mtu mmoja au kwa nia moja...
Ila seriousl, mtoto kama huyo, nawengine wengi walikuwapo kwenye tukio hilo, wanakua na message gani kwenye vichwa vyao?
Wakati nchi zenye vita watu huwa wanakimbilia kwenye nyumba za ibada kujificha, huyu ambaye anakua kwenye nchi yenye 'amani' afu akiwa umri huu tukio la uvunjifu wa amani linatokea akiwa kanisani aeleweje?
Seriously, hao watu waliofanya tukio hili wamefikiria wanayoyafanya...
Tusikubali, kama taifa, kupelekwa huko wanakotaka kutupeleka, as sitaki wanangu wakue kwenye nchi ya aina hiyo...kwanza hatujui hata nia yao, so tusikubali, upendo na mshikamano wetu bila kujali rangi, makabila wala DINI uvunjwe na wasiojua dhamani yake!
Tuesday, March 26
Saturday, March 16
Mapacha wa Zanzibar wamewakilisha!!
Mapacha hawa wanaoitwa Arafa na Aisha, wakazi wa Bububu, wamewakilisha wadau wengine kwenye photoshoot ya kuonyesha watoto toka sehemu mbalimbali duniani wakiwa na vitu wanavyovidhamini zaidi--toys.
Wengine toka Africa ni:
Tangawizi – Keekorok, Kenya.
Chiwa – Mchinji, Malawi.
Botlhe – Maun, Botswana.
Norden – Massa, Morocco.
Kuona picha zote BOFYA HAPA!
Subscribe to:
Posts (Atom)