Sunday, May 10

Happy Mother's Day

Mtoto akiongea na Mungu akamuuliza, “Wananiambia karibu utanipeleka duniani, lakini ntaishije kule wakati mimi ni mdogo sana na sina uwezo wowote?”
Mungu akajibu, “Kuna malaika wako atakayekua anakusubiri atakusaidia kwa kila kitu.”
Mtoto akazidi kuuliza, “Ila hapa peponi sifanyi chochote, nakaa tu na nina furaha kila siku kwa sababu malaika wananiimbia, nikifika duniani itakuaje?
Mungu akasema, “Hata duniani huyo maialka wako atakuimbia na utaona mapenzi yake na utakua na furaha sana.”
Mtoto akauliza tena, “Nitaelewaje lugha ya huko duniani watu wakinisemesha?”
Mungu akasema, “Usiwe na wasiwasi, Malaika wako atakufundisha hiyo lugha taratibu utaelewa, na hata kabla hujaelewa lugha hiyo jua kuwa kila maneno atakayokuambia malaika wako yatakua ni maneno matamu tu.”
‘Na nikitaka kuongea na wewe nitafanyaje?” akauliza tena mtoto.
Malaka wako atakufundisha kusali, na hiyo ndio njia ya kuongea na mimi, kwani nitasikia yote utakayoyasema,” alijibu Mungu.
“Na nani atanilinda?”
“Malaika wako ni wa kipekee, kwani atakulinda kwa gharama yeyote hata kama itasababisha apoteze maisha yake ili wewe uwe salama,” alijibu Mungu , na mtoto akatulia kwa amani.

Ile anataka kuondoka kuja duniani, mtoto akakumbuka, “Ila Mungu, hujaniambia jina la huyo malaika,”
Mungu akamjibu, “Ukifika mwite mama, naye atajawa na furaha isiyo kifani,” halafu akamwachia aende duniani.

*****
Kama wewe ni mama wa umri wowote, wa mtoto yeyote, Happy Mother's Day, na jua kuwa wewe ni Malaika maalum na wa kipekee.

Asante Mama, you are the best.

1 comment:

Anonymous said...

Hapa X anaonekana mpoooleeee.