Wednesday, May 20

Pacha Wenye Baba Tofauti



Huyu ni Jordan, na mama, Mia.

Huyu ni Justin, na mama, Mia.
Mwanadada Mia Washngton na mchumba wake James Harrison walikua watu wenye furaha baada ya watoto waliowasubiri kwa miezi tisa, kuzaliwa wakiwa na afya njema.
Pacha hao, Jordan na Justin walizaliwa miezi 11 iliyopita, wakipishana dakika saba, na hamna mtu aliyehisi kuwa watakua na baba tofauti
Ila mama na baba waliamua kupata ushauri wa kitaalam baada ya kuona mapacha wao wa kiume wanazidi kuwa na sura tofauti kadri wanavyokua.
Vipimo navyo havikufanya hiana, kwani vikaonyesha kuwa uwezekano wa mapacha hao, waliokua kwenye tumbo moja kwa muda wa miezi tisa na kuzaliwa siku moja, kuwa na baba mmoja ni 0.01% .
Si mama tu aliyeshangaa, hadi madaktari wa maabara hiyo huko Texas walishangazwa na majibu hayo, kwani hawajawahi kuyaona, huwa wanasikia tu.Baada ya maji kumwagika ikabidi bibie Mia akiri kwamba wakati yuko na mchumba wake huyo alikua ana-cheat na jamaa mwingine, kusababisha pacha hao kuwa na baba tofauti.
“Nimeshtushwa sana, yani katika watu wote duniani, kitu hiki kinatokea kwangu,” alisema. Ila mchumba wake kaamua kusamehe na kusema yaliyopita si ndwele…na kusema kuwa ana nia ya kulea mapacha hao wote wawili kama wote wake.
Lakini alikiri kuwa ni alijisikia vibaya baada ya kupata ukweli huo, “Itachukua muda kujenga uaminifu kama ilivyokua mwanzo,” alisema.
Wazazi hao wamesama watawaambia hao watoto ukweli kuwa ingawa ni mapacha, baba zao ni tofauti watakapokua na akili ya kuelewa mambo hayo.

Inatokeaje Mapacha Wakawa na Baba Tofauti?
Kuna wakati mwanamke huwa anatoa mayai mawili, toka ovary zote mbili, kwa pamoja. Ikitokea mimba ikatunga wakati huu, ndio wanazaliwa mapacha wasiofanana, au kidhungu wanaitwa fraternal twins.
Kama mnavyojua, yai la mwanamke lina uwezo wa kukaa kwa masaa 24 kabla halijaharibika, na mbegu za mwanaume zinaweza kukaa hadi siku tano ndani ya mwili wa mwanamke.
Hapo ndipo mapacha kuwa na baba tofauti inapoweza kutokea, iwapo mwanamke atalala na wanaume wawili tofauti, ndani ya wakati yai liko tayari, na mayai yakawa yalitoka mawili tofauti, basi kuna uwezekano mkubwa yai moja likapevishwa na mbegu ya mwanaume mwingine, na lingine likapevushwa na mbegu ya mwanaume mwingine. Watoto watakua mapacha na watu watadhani ni wa baba mmoja, kumbe ni baba tofauti.
Ingawa inaonekana kama ni kitu kigumu kutokea, tafiti za karibuni nchini Marekani zinaonyesha kuwa katika seti 12 za mapacha, seti moja ni ya baba tofauti, huku watu wakilaumu mmomonyoko wa maadili kwenye jamii hiyo, sijui hapa kwetu ikoje.

2 comments:

Anonymous said...

Big up sana Jiang!! Mambo si ndio hayo bwana.Kwa kweli hapo, umetugusa;wengi hatuna habari kama mambo haya yanawezekana.Likini sasa DNA itazua mambo.Ubarikiwe kwa kutuhabarisha.

Anonymous said...

wow sikuwahi kujua kama hii inaweza tokea, ila inasikitisha kweli, yani mtoto akijua kua anaemlea si baba yake itamuumiza sana, that's bad kina mama tulitulize jamani au tutumie kinga, mana ukifijifikiria tu wewe na starehe zako za muda unaweza leta madhari na sononeko kwenye familia yako, bora mtu utumie condom kama umeamua kuendekeza ufisadi wa kutoka nje ya ndoa