
Mama na Mwana inasikitika kwa kuondokewa na mmoja wa wadau wake, kipenzi chetu, Diana Onesmo Nathan. Malaika huyu ametimiza mwaka mmoja jana, kabla ya kutokewa na kifo chake leo hii katika Hospitali ya Herbert Kairuki Dar es salaam.
Mama na Mwana inawaombea mama yake na baba yake, Mr & Mrs Onesmo Nathan wa Kimara Bucha Dar es Salaam, Mungu awajaalie moyo wa uvumilivu na ujasiri katika kipindi hiki kigumu.
Mipango ya mazishi inafanyika Kimara mwisho kwa Mzee Kaluse.

Diana (kushoto) akiwa amebebwa na baba yake Onesmo. Kulia ni Glory Mroki. Hapa ilikuwa baada ya kubatizwa Desemba 26, 2008.

Diana (kulia) akiwa amebebwa na baba mdogo Mroki (Father Kidevu) na kushoto ni Glory. "Diana tulikupenda sana lakini Mungu amekupenda zaidi"
RIP Diana.
13 comments:
masikitiko makubwa sana,mungu amlaze mahali pema peponi
Mungu awatie uvumilivu in this trying period, so sad!!!!!!
Rest in Peace,jamani roho imeniuma utafikiri mtoto wangu!!
RIP. she was so gorgeous and adorable and healthy............ mwenyezi mungu naomba umuweke malaika huyu mahala pema peponi.AMIN.
RIP Diana. mungu awape moyo wa uvumilivu wazazi wake, kwa kweli ni msiba mzito sana
Jamani ni majonzi mazito Mwenyenzi Mungu amlaze mahali pema peponi,tunawaombea wanafamilia mwenyenzi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.Amen.
Jamani, jamani ni masikitiko makubwa saaaaaaaaaaaaaaana sina la kusema, Mungu amemuhitaji zaidi ya sisi, amwangazia mwanga wa milele na astarehe kwa amani mtoto wa watu,poleni sana wafiwa.
poleni sana kwa kuondokewa na mtoto wenu mzuri. MUNGU awape faraja.
Jamani.wat a nice baby..it is soo sad jamani. RIP Baby Diana..Wish the parents wapate nguvu na wazidi kumshukuru mwenyezi mungu kwa yote..Mungu anatoa na Mungu anatwaa..
Tunakutakia pumziko la milele Diana.
Mungu awape nguvu na uvumilivu wazazi katika kipindi hiki kigumu.
Ni mimi mama na babay Jerry who everyday have to stop by on "mama na mwana blog"
Mungu awatie nguvu na moyo wa uvumilivu baba na mama Diana kwa kuondokewa na binti yao. Tunaamini Mungu amempenda zaidi kamwita ili aongeze jeshi lake la malaika. Bwana alitoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
Mr. & Mrs. Onesmo, kweli ni ngumu kukubaliana na hali halisi ya kuondokewa na kipenzi chetu Diana. Kimsingi ni kuwa tulimpenda, lkn Mungu nae amempenda sana.
Mungu awape faraja ktk kipindi hiki kigumu.
meen, it is very sad to see a litle one like Diana going too soon like that, what happened to DIana jamani, R.I.P Diana!
Post a Comment