Sunday, January 4

Baby Gadgets - Stroller

Dalvis Mlingi akiwa kwenye stroller yake ambayo mama yake, Joyce Macha, amehakikisha amemetisha rangi.
***
Watu wengi wananunua hiki kifaa kinachoitwa stroller, mi kiswahili chake sikijui, hata Xchyler anayo. Nnachotaka kujua ni, hivi na vumbi letu la bongo, tunakitumia wapi ambako ni salama na watoto wetu hawatamwagiwa mavumbi kifaa hiki?

4 comments:

Anonymous said...

Kwanza hongera kwa kutoka kivingine,kwani imekuwa desturi yetu sisi wabongo kuigana katika kila jambo. Nimeipenda sana blog yako na naifuatilia ingawa bado sijaitwa mama lakini ni mama kwa jinsia. Nimeona swali lako kuhusu stroller au babycar nikapata hamu yakuongea. Kwa mtazamo wangu ni hivi:
Kwa maisha ya tanzania hatuhitaji hiyo kitu kwa watoto wetu ila ni ile desturi yetu yakuiga kila kinachofanywa na watu wa nchi zilizoendelea. Kabla ya kukinunua jiulize maswali yafuatayo ndipo utajua na maanisha nini. Jiulize unapita nayo barabara ipi ambayo imetengenezewa sehemu maalum kwa waenda kwa miguu au ni barabara zipi za mitaani zina lami ili upite bila kuzoa vumbi, na bila kukutana na mawe,maji machafu na mashimo. Je ninapotembea nacho ninakuwa salama mimi na mwanangu?Hii ikimaanisha hali ya usalama barabarani kwa tanzania iko katika hali gani. Ukumbuke unaweza kukutana na gari ghafla kwa maisha ya tanzania limetanua barabara kwa mfano uko ally hassan mwinyi road uko na mwanao na madereva wa kibongo hawajali waenda kwa miguu hata ukiwa kwenye zebra cross .
Matumizi ya hizo baby car kwa nchi zilizoendelea ni rahisi kwa sababu (mfano huku japani ninako ishi mimi), hakuna barabara isiyo kuwa na lami nzuri, barabara zimetengenezewa sehemu maalum za kupita watu na gari haliruhusiwi hata kwa bahati mbaya kupita eneo hilo nikimaanisha sheria za barabarani zinafuatiliwa na ukikosea faini ni kubwa sana ukishindwa kulipa utakwenda jela. Amini kuwa unaweza kumtuma mtoto wa miaka 4 supermarket na akavuka barabara yenye magari mengi kama morogoro road (kwa tanzania) mtoto akavuka barabara vizuri na madereva wakajali usalama wake wakasimama kumruhusu apite. Pia tujiulize ukipanda kwenye daladala na babycar konda anakukaribisha vipi hasa abiria wanapokuwa wengi. Huku unapanda kwenye basi na mwanao umemuweka kwenye babycar iwe kwenye train au bus hakuna atakaye kusemesha kwa sababu inaeleweka matumizi ya hicho kitu.
Kwa mtazamo wangu ni vizuri zaidi kwa maisha ya tanzania ukanunua ile kitu yakubebea mtoto mgongoni au kwa mbele unakuwa na amani zaidi na popote utaenda naye hata kama kariakoo wakati ukitumia hiyo babycar si rahisi kwenda nae huko. Haileti maana kuwa na baby car ukawa unatumia kumzunguusha mtoto akiwa nyumbani tu au ukitaka kwenda kwa mtu tena kwa gari yako binafsi ndio utatumia kumbeba mtoto mkishuka kuingia ndani tena huyo mtu awe ana nyumba sehemu nzuri si eneo lenye mawe na michanga.
By Fatma Ally

Anonymous said...

Some of the content is very worthy of my drawing, I like your information!

Anonymous said...

After reading the information, I may have different views, but I do think this is good BLOG!

Anonymous said...

mie sioni kama hizi vigari vinafaa wka bongo jaamni mwee wanaiga tu ila hawatumii wka raha bali kwa show off . Barabaa hazifai na mabusi yetu ndio kujaa mtindo mmoja mwee huwaga nashangaa wanavyobebelea vitu vya majuu wanatumia kule in wrong way bowa wawekeze hela wka vitu vya manufaa jamani. Haalfu nilicheka rafiki yangu bongo amejifungua hata mwezi mtoto hana amekalishwa kwenye kigali TOBA wakati huku kigari kinatumika in 2 stage miezi 3-6 ya mwanzo analala then atakapokomaa ndio unabadilisha from sleep model to sitting then buggy ya kutembelea mwee