Monday, February 16

Karibu Prez Banda

Mtoto aliyetoa shada la maua kumkaribisha raisi wa Zambia, Banda, wiki iliyopita akiwa amebebwa na raisi huyo. Naamini hii picha wazazi wake wataitunza milele.
picha hii nilipoiona tu, nikasema lazima nmiiwekee mdahalo, maana hiki ni kitu ambacho nimekua nikijiuliza siku nyingi.
Watoto hawa wanatokea wapi na nani huwa anachagua?
Kigezo gani kinatumika kuwachagua? maana mi nawajua watoto wengi tu wazuri, ningependa nijue jinsi ya kuwapendekeza ili wiki ijayo anapokuja raisi wa Turkey nao wapate nafasi hiyo.
Kwa nini siku zote ni wasichana? Ina maana mwanangu Xchyler na uhandsome wake woote hatapata nafasi kama hii ya kumkaribisha rais?
Kama kuna mdau anajua atusaidie, plz.
(Picha hisani ya Anko Michu)

2 comments:

Anonymous said...

kwa uelewa wangu mdogo hao watoto mara nyingi ni watoto wa wafanyakazi wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa.

Anonymous said...

ni kweli kabisa kama huyu ni mjukuu wa mama Ana Kilango malecela ,ni mzuri na mtundu sana anaitwa malaika aka ika.