Sunday, February 15

Maajabu Kwa Wadhungu

Watoto Alfie Patten (miaka 13) ambaye ni baba, na Chantelle Steadman (miaka 15) wakiwa wamemkumbatia mtoto wao Maisie Roxanne aliyezaliwa salama tarehe tisa mwezi huu.
***
Haya yangetokea Mtwara au Lindi wangesema mimba za utotoni zinasababishwa na ukosefu wa elimu, haya sasa yako UK, ambapo watoto hawa wamefanya ambayo kwa uwezo wa miili na akili zao ni bado sana kuyafikia, acha uwezo wa kifedha.
Mimba ya Maisie ilitokana na watoto hao kufanya tendo la watu wazima mara moja tu,(mtoto wa kiume anasema ilikua mara yake ya kwanza) ila bila kinga mwaka jana. Watoto walijua wameharibu baada ya wiki 12 lakini waliamua kutotoa. Wakaficha mimba hiyo hadi mama yake binti alipogundua wiki sita zilizofuata na ikabidi wazazi, ambao wote wanamaisha duni, wakubaliane na hali halisi.
Huyu mtoto-baba anasema sometimes baba yake huwa anampa paundi 10 za matumizi, na hajui nepi zinauzwa shilingi ngapi ila anahisi ni ghali.
Namuonea huruma huyo mtoto aliyezaliwa kwani mtu yeyote mwenye akili timamu ila hasa ambaye amewahi kuwa mzazi anajua kasheshe za kuwa na mtoto. Malezi bora yakikosekana, mtoto ndio anaathirika, Mungu amsaidie malaika huyu, kwa si kosa lake.

3 comments:

Anonymous said...

mh mbona kavulana kadogo sana, ebu wakapime DNA bwana manake nahisi huyu mama anakasingizia katoto ka watu lo

Anonymous said...

kweli kabisa huyo dada ni mkubwa itakuwa amembambikizia.

Anonymous said...

Jamani akina mama inabidi tumwombe mungu sana atuepushe na balaa la watoto wetu kuharibikiwa na kujikuta wakiingia uhusiano na 'mizee' bila kujali kama ni mtoto wa kike au wa kiume.