Monday, February 9

Mdahalo: Diapers zinaleta UTI

Xchyler akiwa anazurura akiwa amevaa disposable diapers, na soksi tu.
***
Wengi tunaziita pampers, ila kiukweli jina lake ni disposable nappies(UK), yani nepi za kutumia mara moja na kutupa au diapers (USA).
Pia wengi tunalalamika kuwa zinasababisha UTI, ingawa wengine hata hatujui kirefu cha UTI ambacho ni Urinary Tract Infection, naomba nisiongee mengi kuhusu hilo, as mi si mtaalam.
Mdahalo wa wiki hii ni kuhusu hizo pampaz kuleta UTI kwa watoto.
Nipeni experience zenu, afu mtaalam atatuweka sawa.

5 comments:

shamim a.k.a Zeze said...

JAMANI ..WADAU MBONA ZIIIII...TUNAHITAJI MAONI YENU MAANA twachanganyikiwa kina sie

Anonymous said...

Zeze kwanza hongera kwa kupata baby girl leo siku ambayo ni birthday yangu. Katakuwa katulivu kama mimi aunt yake teh teh teh

Kusema kweli si kweli kuwa pampers/ dipers zinaleta UTI isipokuwa zikitumika visivyo.

Unajua wengi wa akina mama huwa wanajisahau wakishamvalisha mtoto pempers basi ndo mpaka jioni kwa vile haivuji wanasahau kuwa vijidudu vya uchafu kutoka katika haja ndogo za mtoto hubakia na ndivyo vinavyoingia na kuleta UTI.

Hivyo basi pampers hazijatengenezwa kushindia bali kumvisha sehemu maalumu na kwa muda mfupi.

Mama Raheem.

Anonymous said...

sio mbaya kutumia ila usimvalisha siku nzima bila kubadilisha na pia inategemea aina gani umetumia . HIVi sikuhizi bongo watu wanatumia daipers sio nepi?? na hizo daiper zinauzwa bei gani? nataka kuja holiday sitaki beba mzigo kama zinapatikana huko kiurahisi.

Anonymous said...

we hap juu umeniudhi kweli, bora uulize ndugu zako, utakua umekaa nje mda kweli, anyway ukipata nauli usibebe chochote, there is everything huku sikuizi, watu wanaruka nje ya nnchi kama uchafu, tena ziko pampers made in hapa hapa bongo pia

msidharau bongo, mtashangaa, eti hutokataka kurudi huko kwenye shida

Anonymous said...

jamani kina mama, pampers hazileti UTI, ila ni pale utakapo muacha mtoto na uchafu mda wote, labda ni kinyesi kwa mfano, ndo maranyingi hua na uchafu na bacteria, sasa mtoto wakike kwa mfano, unakuta anakaa na choo mda mrefu mpaka kinaingia sehemu zingine, sasa kama kuna bacteria humo, wanaweza mletea infections ingawa hata wa kiume pia

so sio pampers, hata nepi, sema nepi mana italowa utakumbuka kumbuka kumbadili mapema na mana kwanza utamuona mbichi, pili mtoto mwenyewe anaweza akakukutaarifu kwa kulia mana ubichi unamkera au choo, na mkojo vinamchoma, sasa tafauti ya pampers kwakua inamuacha mkavu, nawewe ukijisahau kumcheki unaweza kuta amekaa na choo for hours

pia kuna diapers kama ponpons, gizmo na zingine nyingi za kichina aina kibao, jamani sio kwamba na haribu soko ila nooooooooo,sio nzuri kabisa unless umpadili mwanao kila baada ya nusu saa ila hazinyonyi vizuri, mimi ni pampers au huggies tu, kama sina hela bora avae nepi tu