Tuesday, March 3

Eti Hata Kidole Kinarithiwa...?

Jamani mdau katuma hii picha, ya malkia Cleopatra akinyona kidola na kuapa kuwa kidole kinarithiwa maana mama yake Cleopatra, Glory Mkwawa, amenyonya kidole hivihivi wakati mdogo. Basi kama kufanana hadi kunyonya vidole, basi balaa.
Mimi sina uhakika na hili, ingawa nakumbuka wadau wawili watatu walishasema kuwa kidole kinarithiwa enzi zileee tunamjadili Xchyler.

No comments: