Monday, April 13

Mahitaji ya awali ya mtoto

MAHITAJI MUHIMU YA MTOTORafiki yangu mpenzi, Hilda Chuma wa WIA ni mama mtarajiwa, na karibu anajifungua, ameniuliza nimpe shoping list ya vitu vya mtoto vya kununua.

Kwa faida ya wadau wooote, walioko kwenye hali kama yake, nimeamua kuweka hii list hapa, wiki hii, ili na wengine wanaotarajia iwasaidie baadhi ya vitu walivyosahau.

Mahitaji haya ni mpaka mtoto atakapofikisha miezi miwili, ila utaangalia mwenyewe unachohitaji. Wadau wangine karibuni mchangie!

Vinavyohusu NepiNepi nyepesi: hizi ni kama vitambaa vyepasi zinazotumika mtoto akitoka kuzaliwa tu, kabla kitovu hakijakauka, dozen mbili zinatosha sana.

Nepi za kawaida: hapa nazungumzia anazovaa mtoto baada ya kitovu kukauka. Uchaguzi ni wako, nepi za kawaida za kufua au za kutupa (pampers, lido…). Kama unatumia za kutupa (disposable) nunua hata mbili kila mwezi miezi mitatu ya mwisho, mtoto akizaliwa huna presha.

Vifutio: sio vya panseli, ila ni kama toilet paper za maji kwa ajili ya watoto, hata kama hutumii kila siku, ila zinasaidia sana wakati flani flani hivi. Ila sio muhimu kama unatumia nepi ya kawaida maana mara nyingi utamfutia hiyohiyo.

Chupi za Plastik au zile plastic za kufunga: hizi ni muhimu kama utatumia nepi za kufua kwani zinazuia mikojo kusambaa kila sehemu nepi ikijaa.

4 comments:

Anonymous said...

hongera hilda kwa kuwa mama mtarajiwa nakukumbuka tulikuwa wote jangwani -by fatma

Anonymous said...

hongera hilda chuma tulikuwa wote bwiru girls
Ruth Kirangi

Anonymous said...

Jiang hizo za kufutia zinaitwa baby wipes maana naona tusiwachanganye wadau kusema zinafanana kama toilet paper za maji.

Jiang said...

asante mdau kwa kunisaidia, kwa kweli watu wasije wakadhani ni toilet papers.