Monday, October 19

Mikanda ya watoto...hasa watundu!

Hii nimetumiwa na mdau Prisca Mbeswa anasema:
Yaani dia kuna sehemu mkienda na watoto hizi belt zinafaa sana.
Assume uneingia na Glad/Jada/Mike/Joline/Xchyler sabasaba (Dar), bila kumfunga belt kweli utatoka nae salama bila kupotezana?

Maana wewe utakua bussy unashangaa na yeye atakua bussy anashangaa kivyake. Hapo vipi?
*****
Kusema za ukweli ukiwa na chautundu kama X huwezi kuenda nae sehemu kama Sabasaba, itakuwa balaa! Alivyoanza kutambaa na kutembea kwa kujishkia tulikua tunamzungushia vitu sehemu ili asitoke, labda stul kwenye kona flan hivi, ila siku hizi kawa janjaful (baba yake ndio anavyosema) hamna sehemu asiyoweza kutoka zaidi ya kitandani kwake! ila mi naona kama hizi belt zitamtesa, maana atakuwa kama ka-mbwa flan hivi, au wadau mnasemaje?

Huyu kakaa chini (I can imegine X wangu, hashindwi kufanya hivyo), sasa sijui hapa utamburuzaaa...?

Hawa inaelekea wamashazoea, maana wametuliaaaa.

Kwa utundu wa hawa, hiyo mikanda naona hata hajasaidia sana, imagine mmoja akienda kushoto, mwingine kulia...

Ila hawa wamependeza! afu nahisi pacha hawa, na mikono wameshikana.

Yale yale, niliyosema mie...

2 comments:

Anonymous said...

Mimi nilipokuja Tz nilitumia mkanda maana mwanangu ni mtundu mno. Ila wa2 wanaonifahamu walikuwa wananipigia na kuniuliza kulikoni namfanya mtoto kama mbwa? Niliwajibu kuwa ni mtundu mno.
Ni uamuzi wa mzazi kununua huo mkanda au la

Anonymous said...

Jiang labda tukusaidie mikanda hii sio kwa ajili ya watoto watundu tuu sometimes inatumiwa ili kuwapatia watoto usalama zaidi hasa wanapokuwa kwenye mitoko maana huku mitaa ya wenyewe mtoto wako akipatikana na tatizo wazazi mtajibu so kuepuka hayo watu huitumia hata kama mtoto sio mtundu.