Sunday, October 11

Mtoto aanze shule lini?

Hello Jiang
Hongera kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutuhabarisha na kutuelimisha
wamama wa leo kuhusu mambo yote yanayohusu maisha ya watoto
Nina jambo ambalo limenitatiza muda mrefu, hivi ni umri gani sahihi wa
mtoto kuanza shule ya awali? na je kawaida inabidi asome miaka mingapi
kabla ya kuanza standard one?
Maana huwa naona huruma sana kukuta
mtoto wa miaka miwili anapelekwa shule saa moja asubuhi (fikiria
ameamka saa ngapi) na kurudi hadi afike nyumbani ni saa tisa. Naomba
utusaidie kwa hapa ikiwezekana utafute mtaalamu wa mambo ya watoto
atufafanulie.

Mungu akubariki sana
Mama Kenneth
http://womenofchrist.wordpress.com/
Wadau toeni ushauri...mimi mwenyewe sijui, huyo X kidogo nimwanzishe mwezi wa tisa huu (sasa ana mwaka 1 na nusu) nikaambiwa sio vizuri, as bado mdogo sana, kwa hiyo nimeona nisubiri hadi mwaka kesho akiwa na mieka miwili na nusu, sijui wenye watoto wakubwa kidogo mnasemaje, maana mlishapitia mambo haya.

4 comments:

Anonymous said...

Watoto kuanza shule mapema ni vizuri hasa kwa mtoto asie na nafasi yakuchanganyana na watoto wenzie. Kama wazazi wote wanafanyakazi, Kwa mfano sasa hivi wazazi wengi hasa kwa wale wenye mwelekeo fulani nyumba ina geti kubwa, mbwa nakadhalika: Hapa hakuna mtoto wa jirani anaeweza kuingia ndani na kucheza na mwanao kwani mtoto muda wote atakuwa na dada tu. Ndo maana wazazi wa aina hii hupeleka mtoto shule mapema.

Ubaya wake watoto wengine huchoka shule mapema, na kuchukia shule katika umri mdogo sana.

Miaka 25 iliopita nilipokuwa mtoto nimecheza sana nje nawatoto majirani hadi nikajua kusoma na kuandika na hata hesabu kabla ya kuanza darasa la kwanza nikiwa na miaka 6 na hii sio kwangu tu ni kwa watoto wengi tu wamtaa nilokuwa nikiishi. Tulikuwa free kucheza hadi barabarani magari hayakuwa mengi ndo tulipata muda wakuandika vihesabu na majina yetu. Dunia ya leo hii thubutu kwani utu umeyeyeuka kila mzazi jicho lake kwa mwanae hakuna atakayekutunzia mwanao tena sana sana ni kumuharibu.

Wataalam wa mambo ya watoto tuhabarisheni ili tupate somo.

Asante kwa mleta maada.

Anonymous said...

Asante kwa ushauri mzuri. Je. mtoto kama kafikisha mwaka na nusu hajaweza kuongea anaweza kumpelekwa pre nursery tena ya English medium??

Anonymous said...

mi naona wakati mwingine ni vizuri kumpeleka mtoto mdogo wa hivyo day care, zipo day care nzuri na wana programm nzuri kwa below 2 years then akifikisha 2 and half hapo wanamweka kwenye play class the pre kindergaten sasa inategemea na mtoto anacatch kiasi gani wengine in 3 years anaweza kwenda lower nursery then 4 year upper nursery as siku hizi five years wanaenda std one. kuhusu kuchoka mi sioni kama wanachoka cz kwa mfano little achievers dsm wana special program kwa age groups so anakuwa na activities kulingana na umri na wanakuwa na muda mrefu wa kulala pia. Mtoto kukaa na dada ni nziri pia but hao dada siku hizi mara yupo mara kaacha kazi unakuta mtoto in 2 years kalelewa na dada sita sidhani kama ni health bora shule mazingira ni more conducive na anakaa na watu professional otherwise watoto wanajifunza zile activities za dada na kulilia mifagio na madekio.

Anonymous said...

yes vizuri akienda shule mapema.Wangu ameanza daycare at 1 yr then 2yrz akaenda pre-kg 3yrz-4yrz kg(kindagarten) nau yupo 5yrz clas 1.amechangamka mno n so bright cz kapata nafasi ya kujimix na wenzie mapema as wel as kujifunza mengi.