Thursday, January 7

Ufafanuzi dawa ya malaria

Wiki iliyopita tulipata taarifa juu ya kuumwa kwa mdau Kelvin Pongo, na dawa ya malaria kumdhuru. Mam'tu, Thecla Timothy aliahidi kutuletea jina la dawa hiyo, na akaifatilia kwa kweli na amenitumia mail anasema kuwa daktari wake amemwambia kuwa dawa hiyo ni nzuri, ila inadhuru baadhi ya watoto, akiwemobahati mbaya mdau Kelvin.
Ningeweka jina ili mjihadhari nayo, lakini haidhuru watoto wote, sasa nnavyowajua watanzania siye, nikitaja jina tu, wote tunaweza tukaikimbia afu nikawa nimeharibu maana dawa nyingi tu zinadhuru baadhi ya watu na wengine zinatutibu vizuri, basi mi naomba tu muwaamini madaktari wenu kwa dawa watakazowaandikia, maana ingekua inadhuru watoto wengi ingeshakatazwa na wizara ya afya.
Hope tumeelewana.
Asante sana Thecla.

2 comments:

Anonymous said...

Pole sana Kelvin. Napenda niwaambie akina mama wenzangu kwamba siku hizi hali ya hewa imebadilika. Watoto wengi wanasumbuliwa na infections. Ukienda kwa madaktari wanasema bakteria ndilo tatizo kwa watoto wengi. Wengine wana infection za kifua, wengine koo, wengine pua na wengine masikio. Kwa ushauri kwa akina mama wenzangu, kuweni macho muwapeleke watoto hospitali. Msijiliwaze na maneno ya mitaani kwamba meno yanaota mkaacha kwenda hospitali. Vile vile muwe macho na hizo homa kwani zinaweza kumletea mtoto dege dege. Tujifunze kukaa na themomether jamani maana inasaidia kupima na kufahamu kama joto utaona linazidi 39C basi ujue hiyo ni hataari lazima umsponge au umwogeshe maji ya bomba. Kisha umpe panadol homa ishuke; vinginevyo, dege dege inaweza kusababisha kifo au ulemavu wa kudumu. Mimi ni mdau

Mama Kelvin said...

asante sana mdau kwa ushauri tutalifanyia kazi na wamama wenzangu kweli tupo hapa kuelimishana zaidi ili tujue jinsi yakuwalea vyema watoto wetu kama ambavyo mdau Jiang ametuwezesha kupitia blog hii.