Thursday, January 21

X akiendesha baisikeli!

Xchyler akiwa anaendesha baisikeli aliyoletewa na bibi...kiukweli wala haendeshi, amekaa tu hapo, na anatetemeka kwa kuogopa kuanguka (ingawa sio rahisi aanguke as ina vitairi vidogo viwili kusapoti tairi la nyuma)...
bib'mtu alivyo na haraka na mjukuu, hii baisikeli aliinunua siku nyingi sana, yani miguu wala ilikua haifiki kwenye peddle, at least sasa hivi inafika, ila kuendesha bado!

11 comments:

Anonymous said...

jianga kazi yako ni kusukuma tu hapo maana ukimzoesha utakoma!! mwambia fundi baiskeli ashushe kiti hadi mwisho atafikia tu sema kuendesha ndiyo hadi azoee!!

msalimu sana X

Anonymous said...

mama x blog yako haina mvuto kila siku picha za birthday tu weka hata lessons mbalimbali,mada,umeanzisha blog ya watoto with no knowledge kutwa x x x.ndio mana hata blog pendwa hazikupi shavu

Anonymous said...

Mh hulazimishwi kuingia hapa.
Hata wewe waweza fungua yako na kuandika kila siku habari zako.

Jiang, kazi nzuri.

UNTOUCHABLE GIRL.

DK said...

Hi Jiang
Huyu mtu ana wivu tena wa kijinga sana na sijui anataka nini hapa kwnye blog hii Takatifu.

Girl - you just continue, what you are doing. We enjoy it!!

From DK

Anonymous said...

nimekupa tu ushauri sasa hayo ya untouhable girl yametoka wapi uswahili tu.

Anonymous said...

mdau hayo ya uswahili wala hayajaanzishwa na Untouchable girl, soma comment yako mwenyewe ndio utaona ulivyotoa ushauri kiswahili maana umesema 'umeanzisha blog ya watoto with no knowledge kutwa x x x.'kama si uswahili ni nini?
sasa ulidhaini uswahili unaujua peke yako?
kama unatoa ushauri fanya kistaarabu,
ukileta comment za kiswahili, tunajibu kiswahili vilevile!

Anonymous said...

Annony wa pili umenikeraaaaa! blog pendwa hazimpi shavu mama x kwani ye kakwambia anataka shavu blog pendwa?
usidandie tren kwa mbele wala hujui lilikoanzia hii blog isharushwa sana kwa michuzi, au we unazungumzia blog pendwa zipi?
eti huna knowledge, wewe ndio huna knowledge, maana hata huelewi maana ya tabs zilizopo kwenye hii blog, uone lessons na mada zilizowahi kutolewa na kuchangiwa kabla hujaanza kusema eti ooooh, umeanzisha blog wakati hujui... watu wengine hovyooooooooooooo!

Lulu said...

Jiang!!! Weka picha kama kumi hivi za X na za wadau wengine pia tena za birthday, ubatizo, maulid na matukio mengine ya watoto. Huyo anayetaka knowledge aanzishe blog yake aweke knowledge zake hapa unafanya unavyotaka wewe siyo anavyopenda yeye. Haya kanyaga twende Jiang!!!!!!

mdada said...

Akhu mwenzangu jiang usijali maneno yetu wabongo,wengine tunapenda kuingia hapa tuone watoto wanavyokua,as tumewaona toka tuchanga.endelea dada.By the way hii ni blog yake mwenyewe alianzisha baada ya kujaaliwa X,soo why not X X X.Halo

Anonymous said...

Kila blog ina theme yake, Nadhani tangu mwanzo Jiang aliweka wazi kuwa anataka ku-share na watu wengine vile X anavyokua lakini amekaribisha wadau wengine wanaofanana na X, nikiingia hapa napata mambo yanaendana na akina X, na nikiingia blog ya fashion napata vinavyoendana na fashion, au malavidav, misosi, nk, so lazima tuelewe jamani kila mtu ananzisha kitu vile roho yake inapenda...banafsi naifurahia mama na mwana jinsi ilivyo, mada zinazohusiana na watoto, watoto wenyewe picha za mama na baba inapendeza. Uko juu sana mama X, Congrats. mama R

Anonymous said...

Kanyaga twende mama x speed 180 acha huyo mshamba akafie mbele yani kama una idea yako tofauti na mama x usihangaike kuangalia hii blog anzisha yako usitake mawazo yako ya knowledge hapa na knowledge yenyewe huna. sorry ur in a wrong place wewe uliyecomment kila siku x x x