Tuesday, May 18

Karibu Baraka

 Jana tu nimeulizia baby no 2, nimepata jibu toka kwa Edda Mmasi, anasema yeye tayari keshatuletea mdau wa pili.
Malaika huyu mpya, anaitwa Baraka, amezaliwa Ijumaa ya tarehe 30 April.

Cuuuuuuuuuuuuuuuuuute!
Alizaliwa kwa operation, maana alikua 4kg, Mungu amejalia, mdau na mama, Edda Mmasi wanaendelea vizuri. Kaka yake mkubwa anaitwa Prince, ni mdau wa siku nyingi sana hapa kwenye playground yetu.

Hapa kaka mkubwa akinywa soda kwenye sherehe yake ya kutimiza miaka miwili, ilikua February 2.

tam tam ya pool table...

Party ilikua home, then akaenda kujivinjari South beach, kama anavyoonekana hapo chini...

Miwani imemtoa bomba!
*****
Mama na Mwana pamoja na wadau woooote tunampongeza mamie Edda kwa kuleta mdau mpya wa kucheza naye hapa kwenye playground yetu, pia tunamuombea mdau mpya Baraka, Mungu amjaalie afya njema na maisha merefu yenye kheri na baraka tele amzidi hata wa jina wake Baraka Obama.

No comments: