Tuesday, June 19

Haki 7 za mama mjamzito


1. Mama mjamzito ana haki ya kupishwa akae, hata kama amechelewa kufika eneo la tukio, na nyie wengine mmegombea hizo siti, mpisheni tu!


2. Ana haki ya kudondosha kitu na kusubiri mtu ajitokoze kumwokotea!

3. Ana haki ya kudai umiliki wa chakula cha aina fulani ndani ya nyumba. Yaani hicho chakula kikiingia tu, hata kama amekuja nacho mgeni, inabidi aki-surrender kwa boss! Na ole wake atakeyechukua kile cha mwisho kilichobaki, afu mwenyewe aamke saa 9 kukitafuta, siku hiyo ndio mtajua nani ni boss!4. Ana haki ya kusahau vitu na kusingizia mimba…it has been scientifically proven kwamba mtu akiwa mjamzito anasahau sahau, sasa kama anajifanya au kweli, imekula kwako!

5. Ana haki ya kulalamika au kuguna anapofanya kitu chochote, hasa kinachohusisha kunyanyua huo mwili, kwa usalama wako wewe msaidie tu!

6. Ana haki ya kutuma mtu, hasa baba mtarajiwa kumchukulia kitu chochote, sehemu yeyote na saa yeyote…tafadhali baba, kwa usalama wako zingatia maelekezo, kama ni bugger za science afu ukaleta za Morocco, yatakayokukuta, mie simo.

7. Ana haki ya kulia saa yeyote, kwa sababu yeyote, na hata kama unaiona ya kijinga na kitoto, keep your opinion to yourself, as akikusikia unamsema, utasababisha kilio zaidi! Jamani, wanasayansi washasema mjamzito anakua emotional sana, so she cant help it!


Ni hayo tu, kina baba na kina mama kuna ambalo mjamzito hana haki nao hapo juu? Je una haki ya kuongezea; share na sie hasa kwa faida ya wajawazito wote na utawaokoa sana kina baba watarajiwa kwa kuzijua hizi haki. Tupia comment yako hapo chini.

3 comments:

Anonymous said...

mjamzito ana haki ya kwenda klinik na baba

Anonymous said...

HEHEEEE NIMECHEKA JAMANI NA KUMBUKA ENZI NZILE.MR HUWA ANANIKUMBUSHA VITUKO MBAKA NA CHUKIA HUWA NAJIULIZA NI MIMI KWELI NDO NILIKUA NAVIFANYA.MIMBA ZINAVITUKO

Anonymous said...

Ha ha ha ...mi nicheke tu niongeze umri wakuishi...wanawake kwakudeka!!