Sunday, May 9

Nani kama mama?

Happy Mother's Day kwa wadau wooote wa Mama na Mwana, nina imani kwamba mmepata muda wa kuwapa heshima mama zenu, kupitia sikukuu hii ambayo ilianzishwa maalum kwa ajili hiyo.
Tofauti na sikukuu nyingine, hii sio sikukuu ya wingi, ndio maana ni Mother's sio Mothers day, nia ikiwa ni kila familia kusherehekea sherehe hii kwa kumkumbuka na kumshukuru mama yao.
Hivyo basi nachukua nafasi hii kumshikuru na kumwambia mama yangu kwamba nampenda sana.
Mama, wewe ndio mwongozo wangu katika kila nnalofanya, na  nashukuru kwa kuwa na wewe kama mama yangu, Akhsante mama.