Thursday, June 10

Mdau ameleta utata siku ya Stars na BrazilKuna watu wanasema ametia aibu maana hatulii, ingawa wanasema wa kulaumiwa ni TFF kwa kuchagua mtoto mdogo hivyo, wengine wanaona poa tu, kwa kua alikua wa UKWELI, yaani haigizi anafanya vitu kitoto kweli...mi naona alikua poa, tena alichangamsha sana...wadau mnaonaje?
Nimeambiwa hawa watoto walitoka kituo cha kulelea watoto cha SOS Village, maana watu walishaanza...

10 comments:

Anonymous said...

Nilimpenda sana,, yupo kiukweli na nimchangamfu, pia ameonyesha mapenzi yasio ya kuigiza, kama ni mtoto wa kitua basi amepata malezi ya mazuri na wapongeza.
Mara nyingi tunapenda watoto wetu wa pretend kuwa namna ambayo sivyo walivyo na hii nafikiri inawazuia kuibua mambo mazuri yakwao kama wao.

Anonymous said...

so adorable boy, he's so innocent. i real love him.

Anonymous said...

Mi hata sioni kibaya alichofanya,km ambavyo blog za tz zimeandika,huyu ni mtoto na always mtoto hawezi kupay attention kwenye kitu chochote kwa zaidi dakika5,afterall hakuonyesha utundu zaidi ya mapenzi kwa huyo mchezaji.

Anonymous said...

Hao wanaosema ametia aibu ndio wanafiki wanafundisha watoto wao uongo. The boy was innocent and marvelous. Hakuna kupretend, nimemfagilia asilimia 100. Kama angekuwa amefanya jambo baya hata hao wafaransa sijui wasingemuonesha lakini it's interesting ndio maana wameirusha na unaona hata sura ya mtangazaji inasomeka it was a funny thing.

Love you baby

Anonymous said...

Jamani mie nilivyoona hiyo clip, nimecheka mpaka basi, yaani mtoto wa ukweli! Nafsi yake safi, malaika wa Mungu hana moja alijualo duniani, halafu ukiangalia vizuri clip hata hao wachezaji wa Brazil walikuwa wanacheza naye kwa kumdokoa dokoa nafikiri walikuwa wanapenda alivyo mcheshi, I wish ningesikia hicho kispanish lakini ntatafuta mtu anitasfirie. Mwisho nilicheka zaidi pale alipopewa mkono na Mhe. Rais wakati mkono wake kaufunika na Tshirt yake sijui alifanyaje? I wish wangeonyesha mpaka alipompa mkono Rais. What an angel! So cute,and innocent.

Hao wanaomponda na kudai sijui nini ndio wanafiki hao, hao ndio wale wakifika kwao wanafikia hoteli, wakiona picha za kijijini kwenye mablogu wanachefuka na kuona aibu! Wapi bwana hapa duniani ni mapito tu, I wish ningerudi nikawa kama mtoto kama malaika.

Bi Mkora

Anonymous said...

dada,na yule mtoto wa kizungu katika iyo aparade na yeye katoka SOS village (mtoto yatima?)iki kituo kinachukua watoto yatima mataifa mbalimbali???

ni hayo tu

Anonymous said...

KWA KWELI HUYO MTOTO I WISH ANGEKUWA WA KWANGU KWANI NI MCHESHI NA ANA UNAFIKI WA ROHONI YAANI HATA BABA YAKE AKIONA NI RAHA TU WEWE WA BRASIL ONA WALIVYOKIFURAHIA EBU JIULIZE HUYU BABE NI WA NANI ,??? SO FUNNY !

Anonymous said...

dears,wala msiumize kichwa...
hao wanaosema huyu mtoto ametia aibu sidhani kama wana akili timamu,
hayo yoote ni matendo ya kila mtoto wa umri wake.. na wala hawa wabrazil hawalaumu hicho zaidi ya kusema he is adorable!!

kama kuna limtu linasema vinginevyo huyo ni mnyama!!

Anonymous said...

bravo mtoto mzuri kweli huyu,hao watu ni wajinga wanaosema mtoto kaaibisha,hata wachezaji wenyewe walikuwa wanacheza nae na halafu walimchokoza.

Anonymous said...

Ndio maana wanaitwa watoto kwa kua ni malaika wa mungu wanafanya kile wanachopendana, anayelaumu hana mtoto siku akibarikiwa ataelewa raha za utoto ni nini?

kuna mtoto mmoja aliwahi kumyanganya malkia wa uingereza mauwa aliyopewa na mwalimu wake, lakini malkia na mapolisi wake wakacheka na kufurahi wakamwachia hayo mauwa na mtoto akatoa kicheko cha furaha, na vyombo vya habari vyote vikafurahia tendo la mtoto alivyo malaika hajali wewe ni malkia au nani.