Friday, July 2

X alikua Sabasaba leo

Xchyler alikua Sabasaba mchana wa leo...niliamua kumpeleka leo kuepuka mrundikamano wa watu wakati wa wikend. Leo ilikua raha as watu walikua wachache, hivyo kutumia muda mfupi kupita mabandani, ingawa pia hatukuingia yote, ila mdau alifurahi kushangaashangaa.

...hapa anataka nimnunulie pilipiki...

Hiki ndio kilikua kituo kikuu...banda la wizara ya maliasili na utalii...alianza kwenye sanamu ya ukweli ya somba na chui!!!

hapa kwenye kobe wakubwa...Xchyler aliwapenda akang'ang'ania awaone kwa karibu!!! alimwita mwangalizi wa pale "ako, oooba, ako oooba"

hadi akakubali kumwingiza ndani ya ukuta wa kobe!!!

 X alipata bahati ya kukaa karibu na kobe hawa wenye umri miaka 150 kila mmoja (wanaishi hadi miaka 300, kwa hiyo hao bado vijana sana)...kwa juhudi zake binafsi...am so proud of him, ila aligoma kuwakalia juu!!!

kiukweli maonyesho hajajachangamka sana, ila kwa mtoto kupata mtoko ni raha sana kwake na yeye ataona vitu vingi vipya kwa hiyo pelekeni watoto wakafurahi!!!

3 comments:

Anonymous said...

MAMA X, MI NAOMBA TU UBADILI PICHA YA PROFILE, HIO YAKO NA MWANAO, IMECHOKA BWANA BADILI MI SIIPENDI HAINA MVUTO. NI USHAURI TU

Anonymous said...

JAMANI KWELI INAFAA KUPELEKA WATOTO HASA KWENYE BANDA LA MALIASILI. ILA SABASABA MI NAONA VITU VYA HOVYO BEI ZILE ZILE AU JUU ZAIDI YA MADUKANI.

UNLESS KAMA MTU UMEFATA CONTACTS ZA WAFANYA BISHARA OTHERWISE KAMA NI KUNUNUA HAMNA LA MAANA.

ALL IN ALL NI FAMILY GET AWAY TU KUTOKA NA WATOTO WAKAOSHE OSHE MACHO

Anonymous said...

Mzee wakunyumba jamani umekuwa kweli kweli. ni kweli ni sehemu nnzuri sana kwenda nawatoto na wao wajionee na wanapata kujifunza mengi