Sunday, November 28

Mwanafunzi afa baada ya kucharazwa viboko

MWANAFUNZI wa kike wa darasa la sita, amekufa kutokana na madai ya kupigwa viboko na mwalimu wake aliyekuwa akimtuhumu kufeli jaribio la hisabati.

Mwanafunzi huyo (jina limehifadhiwa) aliyekuwa akisoma Shule ya Msingi Mawenzusi wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa, alifikwa na mauti hayo juzi katika Hospitali ya Dk. Atman alikokuwa amelazwa kwa matibabu.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu kutoka mjini humo, Kamanda wa Polisi, Isuto Mantage alidai mwanafunzi huyo alipata kipigo hicho Novemba 16, mwaka huu.

Alidai kuwa siku ya tukio mwalimu wa somo hilo, Richard Langson (23) aliingia darasani na kutoa jaribo la hisabati na kuwaonya wanafunzi wake kwamba atakayepata alama chini ya asilimia 70, atapata adhabu ya viboko. 
Jamani, mi viboko sijawahi kuvipenda, na wala sivipendi, hasa vinapokua havina nia ya kufundisha bali kukomoa, naona tu tuanzishe kampeni viboko vifutwe mashuleni, kama watoto hawasikii basi, hasara kwetu wazazi sio kutuulia watoto wetu!!!

1 comment:

Anonymous said...

Nasikia uchungu sana, kwani nawaza mie mnyonge nani atanisikiliza? Nawaza nina katoto kangu darasa la kwanza kakirudi kamekasirika nasikia vibaya sana,ila siku atakaponionesha kapigwa na hao walim feki nadhani unyonge ndo utakapoishia.

Wazazi tuwe na ushirikiano mfano kuandamana kupinga hiyo adhabu kali kwa watoto wetu.

Sitasahau nikiwa primary Shule fulani Iringa, kulikuwa na mwalim aliependa kupiga vibao watoto tena wa darasa la kwanza na mimi nilisha wahi kuwashwa vibao viwili na huyo mwalim.

Kutokana na kipindi hicho kuwa adhabu kama hizo ni haki au tulistahili na wazazi wangu kuwa wapole kupita kiasi na kutojua waende wapi.

Nilimchukia mwalim huyo hadi leo. Kuna siku aliwapiga wababe, basi wakamvizia gizani wakamuonesha kazi.

Sheria ifuate mkondo wake na sina huruma kwa adhabu yeyote itakayotolewa kwa huyo mwalim asiye na wito wa kazi yake.