Monday, April 4

Traffic wanafunzi...


Huu mradi, wa wanafunzi kuwavusha wenzau umeanza hivi karibuni, sijui kama unafanywa miji yote, ila Dar ndio huu hapa...hapa ni Mbuyuni, karibu na Mbuyuni Primary School, na hawa ni wanafunzi wa shule hiyo wakiwavusha wenzao wakisaidiwa na traffic police wa ukweli.
Wanaanza saa moja hadi saa mbili asubuhi...
Ila kuna watu hawaipendi hii program, wakisema inawatumikisha watoto...mnaonaje: watoto wanatumikisha au wanafundishwa kuwa responsible kwa mambo yanaowahusu?

1 comment:

Anonymous said...

Safi sana ni maendeleo mazuri ya nnchi yetu nilizoea kuona hivyo apa dk. natumaini madeleva wetu wataheshimu huu utaratibu wa wanafunzi.
asante Mama X.