Wednesday, February 29

X ingizo jipya!

New family member anaitwa Xyleen Lerato Mapunda...hii ni few minutes after birth!
During my time out nimeleta kitu kipya! Huyu ni mdogo wake Xchyler, anaitwa Xyleen (tamka Shyleen) kifupi ni Xy (Shy). So unaweza kuniita 'Mama X squared'.

Kaka mtu, aka Biggie aka X anampendaaaaaa balaaa...! I know for sure anampenda kuliko mtu yeyote!


X alikuwepo tangu mwanzo, alikua anamsubiri kwa hamu huyo mtoto...


Safari yake ilianzia wakati uleeeee nikiwa SA, so ndio maana tukampa jina la kati  la Lerato lenye sili ya ki-Tswana lenye maana ya pendo.
...Pozi la tumbo....Bize hadi siku ya mwisho...
 Hii ilikua kama siku tatu before kumpokea mgeni huyo...nilienda kazini hadi Ijumaa, Jumamosi mchana nikaenda hospitali, nikajifungua usiku wa kuamkia Jumatatu.

Binti shashiriki matukio mengi ya kifamilia, ikiwamo hii graduu ya dady...
 Kuna walionitumia msg kuuliza kama huyo hapo ni X, yes, ni yeye akiwa na memba mpya wa familia, wakimpa tafu dady kwenye mahafali. (Huyo ni classmate wa dady, Hoyce Temu).
anapenda sana kucheka.

Leo anatimiza miezi sita ya kuzaliwa, so alizaliwa August 29, 2011. Ana kajino kamoja, hiyo picha ya kajino bado sijaipata, maana ni la chini, so kulipata kwenye pozi si kazi ndogo! Katika miezi sita hii kuna mengi ya kusema juu yake, ila mtamjua tu taratibuuu...


...na hapa kwenye bembea yake humtoi!

Of all the things anapenda kula, anything, ila haswa nyonyo!!!
hapa na dady home...

Nashkuru Mungu nimepata shost wa ukweliiii...swali ni nimejizaa au sijajizaa???

Mdau na wewe una update? Iwe la mdau huyo huyo wa zamani tunayemjua au una ingizo jipya we tuma kwenye mamanamwana@gmail.com, maana nimewamisi wadau wangu balaaa!

5 comments:

Kamongo said...

Nilitaka kustuka inakuaje hii au ndo kale kawimbo. Maana baba Black mama Black halafu mtoto anazaliwa mweupe. Au ndo Jiang ulikuwa unakula sana machungwa nini ...lakini hapo chini rangi imeanza kubadilika na jkuja ya halisia. Big up 6-tusi. Ji-young.

Anonymous said...

Hongera sana mama X-square! Yaani nilihisi tu huyu mama na mwana kimyaa atakuwa anatuletea baby!! Afadhali umerudi kwa game tulikumissjee jamani. Hongera sana.

Anonymous said...

Hongera sana Jiang na sixtus

Anonymous said...

hongera bidada, du umepata ka schana na kweli ni shosti wa ukweli. MOLA AKUKUZIE

Royal Curtains Designs said...

Awwww i wish motto wangu angepata birthday mate wa kwanza it is only one day behind Xyleen alizaliwa. My Ethan was born Aug 30